Kikosi cha Yanga |
Ushindi huo umnewafanya vinara hao kufikisha pointi 56 ambazo zinawaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji lake la 23 la Ligi Kuu kutokana na ukweli ni Azam pekee inayoweza kuzifikia pointi hizo ikishinda mechi zake zote, wakati Yanga ikiwa bao na mechi mbili mkononi.
Hata hivyo Yanga inawabidi wasubiri kuanza kusherekea ubingwa huo ambao ni dhahiri ni wao msimu huu mpaka jumamosi kusikilizia mechi ya Azam na Coastal Union itakayochezwa mjini Tanga.
Iwapo Azam italazimishwa sare yoyote basi itatoa fursa ya wana Jangwani kusherehekea ubingwa wa 23 wa Ligi hiyo bila kushuka dimbani.
Mabao yaliyoihakikishia Yanga ushindi huo na kuifanya ilishike kombe la ubingwa kwa mkono mmoja, yalitupiwa kambani na Simon Msuva dakika moja kabla ya mapumziko.
Hamis Kiiza Diego aliiandikia Yanga bao la pili kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na David Luhende katika dakika ya 58.
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliiongezea Yanga bao la tatu kwenye dakika ya 62 na kuwafanya maafande wa JKT Ruvu kupoteza dimbani.
Kipigo hicho cha leo kimezidi kuiweka pabaya JKT Ruvu ambayo inanolewa na kocha Kennedy Mwaisabula aliyechukua nafasi ya Charles Kilinda katika eneo la hatari la kushuka daraja.
Timu hiyo iliyopo nafasi ya 11 ikiwana pointi 23 inahitajika kushinda mechi zake tatu zilizosalia iwapo inataka kuepuka kushuka daraja.
Maafande hao wamesaliwa na mechi dhidi ya African Lyon mechi itakayochezwa Jumatano kabla ya kuvaana na Prisons Mbeya kisha kumalizia na Mtibwa Sugar.
Msimamo Kamili wa Ligi Kuu baada ya mechi ya leo:
P W D L Gf Ga Gd PTS
1. Young Africans 24 17 5 2 44 13 +31 56
2. Azam 23 14 5 4 41 19 +22 47
3. Kagera Sugar 23 11 7 5 26 18 +8 40
4. Simba 22 9 9 4 32 21 +11 36
5. Mtibwa Sugar 24 9 9 6 27 24 +3 36
6. Coastal Union 23 8 9 6 23 20 +3 33
7. Ruvu Shooting 23 8 6 9 21 22 -1 30
8. JKT Oljoro FC 24 7 7 10 22 28 -6 28
9. Tanzania Prisons 24 6 8 10 14 21 -7 26
10.JKT Mgambo 23 7 4 12 15 23 -8 25 11.Ruvu Stars 23 6 5 12 19 37 -18 23
12. Toto Africans 25 4 10 11 22 33 -11 22
13. African Lyon 23 5 4 14 16 35 -19 19
14. Polisi Morogoro 23 3 10 10 11 21 -10 19
No comments:
Post a Comment