Carlos Tevez akiwania mpira na mchezaji wa Tottenham Hotspur jioni hii |
Mabingwa hao watetezi wamediwa na wapinzani wao wa jiji la Manchester kwa pointi 13 katika msimamo zote zikiwa zimecheza mechi 33 na kuifanya Man United kuhitaji kushinda mechi yake ya kesho dhidi ya Aston Villa kutangaza ubingwa huo ikiwa ni mara yao ya 20 katika historia.
Wageni walianza makeke kwa kuwashtukiza wenyeji wao kwa bao la mapema la dakika 5 lililotupiwa kimiani na Samir Nasir na kulifanya lidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Hotspur kucharuka kutaka kusawazisha.
Hata hivyo Tottenham iliingisa kipindi cha pili wakiwa kama mbogo wa kuwakimbiza wageni wao kwa muda mrefu kabla ya kuandika bao la kusawazisha dakika ya 75 lililofungwa na Clint Dempsey kabla ya dakika nne baadaye Jarmain Defoe kuongeza la pili.
City wakijiuliza jinsi ya kusawazisha bao hilo ili angalau kupata sare ya mabao 2-2, winga nyota na mmoja wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo, alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu dakika ya 82.
Ushindi huo umeifanya Hotspurs kufikisha pointi 61 ikilingana na Chelsea ambayo jioni hii inatarajiwa kuvaana na Liverpool katika pambano jingine linalosubiriwa kwa hamu katika ligi hiyo ya England.
No comments:
Post a Comment