STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 27, 2013

Simba yatishiwa Polisi, Machaku aapa Mnyama lazima akae


Kikosi cha Simba
Machaku Salum 'Balotelli' wa Polisi Moro
LICHA ya kuhitaji miujiza ili kubaki kwenye ligi kuu ya Bara msimu ujao, wachezaji wa Polisi Morogoro wana imani ya kujikwamua na janga hilo kwa kuanzia na kuifunga Simba katika mchezo baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa kesho.
Polisi Morogoro ni ya pili toka mkiani katika ligi ambayo zitashuka timu tatu za mwisho, ikiwa na pointi 19.
Ili kubaki kwenye daraja hilo la juu zaidi Polisii nahitaji kushinda mechi zake tatu zilizobaki ili kufikisha pointi 25 na kupunguza tofauti ya magoli ya -10 iliyonayo.
Bahati mbaya kwa Polisi, hata hivyo, jumla hiyo imeshafikiwa na ama kupitwa na timu zote zilizo katika eneo la salama la kubaki kwenye ligi kuu na zikiwa si tu na michezo iliyobaki bali pia uwiano bora wa magoli.
African Lyon na Toto Africa nazo zina uwezo wa kufikisha pointi 25 lakini kwa kubakiwa na michezo miwili na mmoja, kwa mpangilio huo, zipo katika mazingira magumu zaidi ya Polisi Morogoro.
Mmoja wa wachezaji wa Polisi Salum Machaku alisema licha ya timu yao kuwa katika eneo la hatari, lakini hawajakata tamaa.
Amedai wachezaji wote wamejipanga kufanya kweli katika mechi zilizosalia dhidi ya Simba, Kagera Sugar na Coastal Union.
"Hatujakata tamaa na wala hatuamini kama Polisi itarudi daraja la kwanza," alisema na kueleza zaidi, "tumejipanga kupigana kiume katika mechi zilizosalia ili kubaki na Simba wakae chonjo kwani tutakufa nao Uwanja wa Taifa."
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Simba na timu za Pan Africans, Azam na Mtibwa Sugar, alisema hakuna mchezaji wala mwana Polisi Moro anayetaka kusikia habari za kushuka daraja japo wamechelewa mno kuzinduka.
Machaku alisema ugeni wao katika ligi wakati wa duru la kwanza lililosababisha wapoteze mechi na pointi nyingi ndiyo iliyowagharimu kabla ya kuzinduka katika duru la pili wakiwa wamechelewa.

No comments:

Post a Comment