Jonas Segu akimuadabisha mpinzani wake |
Segu akimkong'ota m,pinzani wake |
TANZANIA imetengeneza historia mpya kwenye
ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa wanapigwa kila
mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. Safari hii JEMBE,
kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas Segu kutoka katika
ukumbi wa mazoezi wa Respect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya
kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi
alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa Thailand pamoja na nchi za
ukanda wa Indo-China.
Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF
katika mara la Asia Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand
katika uzito wa Light Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani
katika viwango vya IBF. Mpambano wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya
dhahabu la Bangkok na kurushwa na television katika nchi zote za ukanda
wa Indo-China za Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand
yenyewe.
Mpambamo wa Segu na Pathompothong
ulianza kwa bondia wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na
kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito ya kumshikisha adabu.
Segu alitupa makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong
kutokana na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya
kwanza ilimbidi Pathompothong ajilinde na kukimbia akizunguka ndani ya
ulingo ili kudhoofisha masumbwi ya Segu aliyekuwa anayachanganya kama
mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!
Jonas Segu alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George
“Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye
mpambano huo wa mwaka. Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati
wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda
Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa
makondde mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao
ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong
kutafakari namna ya kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli
alionekana kuwa alienda Thailand kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na
sio kufuata ulaji!
Raudi ta 5 Pathompothong
aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na
kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kenye kamba ili
amkandamizie masumbwi yake. Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura
nzuri ya kuvutia na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na
hoteli aliyoshukia ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha
Pathompothong kuwa yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya
mazoezi ya kutosha. Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo
na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama
vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania!
Katika raundi ya 6 mabondia wote
waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko
(combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani mwenza. Ni katika
kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong.
Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya
nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa
dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa
anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati wa kitanzania.
Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa hawezi kuutumia mkono wake
vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa anaacha!
Segu aliacha pambano hilo katika raundi
ya saba wakati mashabiki wengi katika ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania,
Tanzania, Tanzania kwa jinsi alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania”
No comments:
Post a Comment