Jengo la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere linavyoonekana kwa mbali |
NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wanafunzi wa Kiislam Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere (MSAM) kilichopo Kigamboni Jijini
Dar es Salaam unaomba wadau mbalimbali
kujitokeza katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kiislam wanaomaliza chuo ambayo
yataambatana na harambee ya uchangiaji
wa fedha za ujenzi wa msikiti chuoni hapo.
Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa MSAM Abdullatif
Jafari wakati akizungumza na mwandishi wa habari hivi karibuni Jijini Dar es
Salaam.
Jafari alisema chuo kimewapa
ruhusa ya kutafuta mdhamini wa ujenzi wa msikiti kwa kipindi kirefu ila
hadi sasa hawajapata mafanikio kwani baadhi ya wahisani wamekuwa wakiaahidi
bila mafanikio pamoja na ukweli kwamba MSAM imekuwa ikiteleza maagizo yao kila
wanapohitaji.
Alisema matarajio yao ni kuhakikisha kuwa wanapata kiasi cha
shilingi milioni mia moja za kuanzia ujenzi hivyo basi wanaaomba watu wenye nia
nzuri kwa vijana wa kiislam wanaoishi maeneo ya chuo waweze kufanikisha zoezi
hilo mapema.
Katibu huyo alisema wanafunzi wamekuwa wakichanga mara kwa
mara ila juhudi zao zimekwama hivyo wanaomba mtu, taasisi yoyote yenye uweze kuwasaidia
ujenzi wa msikiti huo ili waweze kumuabudu mungu kwa amani na kwa wakati.
’’Jumamosi ijayo tunawaaga wenzetu wanaomaliza hivyo basi
tunataka kutumia fursa hiyo kuweza kuchangisha fedha za ujunzi wa msikiti
nadhani nao watakuwa wameacha alama Fulani katika haarakati hizi’’, alisema.
Jafari alisema iwapo tutapata ushirikiano kutoka kwa wadau
mabalimbali nchini tunaamini kuwa upo uwezekano mkubwa wa kufanikisha zoezi
hilo mapema na dhana ya kufikiria mtu mmoja tutaondokana nayo.
Alisema ni vema jamii ikatambua kuwa kufanikisha ujenzi huo
itakuwa imechangia msaada mkubwa katika kujenga imani na maadili ya vijana
ambao wanasoma katika chuo hicho cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Aidha Katibu huyo alitoa rai kwa wale wote wenye nia ya
kuchangia ujenzi huo wa msikiti na hawataweza kufika wanaweza kutoa michango
yaao kwa njia za M Pesa 0766656730, Tigo Pesa 0713774828 au akaunti namba ya
jumuiya Muslim Students Association of Mwalimu Nyerere (MSAM) 3300825636 Kenya Commercial
Bank Samora Avenue.
No comments:
Post a Comment