STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 18, 2013

Yanga yazima ngebe za Simba, Toto, Polisi zaungana na Lyon kushuka daraja

Kipa Ally Mustafa 'Barthez' alkidaka penati ya Simba

Didier akishangilia bao lake dhidi ya Simba leo

LICHA ya kutimia ahadi ya kuibuka na ushindi mbele ya watani zao, Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga imeshindwa kulipa kisasi kwa Simba.
Yana iliyonyukwa mabao 5-0 msimu uliopita na kujitapa kwamba leo ni lazima ingelipa kisasi imeishia kushinda mabao 2-0 na kunogesha ubingwa wao.
Mabao ya kila kipindi yaliyofungwa na nyota wa kimataifa wa Yanga, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza 'Diego' yalitosha kuzamisha jahazi la Msimbazi ambao walipoteza pia penati waliopata.
Kavumbagu aliiandikia Yanga bao la kwanza dakika ya nne kwa kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima kabla yha Simba kupata penati baada ya Ngassa kluchezwa rafu na Mussa Mudde kushindwa kuukwamisha kwa kumlenga kipa Ally Mustafa 'Barthez'.
Bao la pili lilitupiwa kimiani katika dakika ya 63 na Kiiza baada ya kuunganisha krosi iliyomkana na mpira wa kurushwa wa Mbuyi Twite na mabeki wa Simba kuzembea kuruka na Kiiza kufungwa kwa kichwa na kuiandikia Yanga bao lililokata ngebe za kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' aliyedai wangeifunga Yanga iwe isiwe kwa ubora wa kikosi chao.
Julio akizungumzia mechi hiyo alisema wanakubali kipigo, lakini wamefurahi kwa kushindwa kulipa kisasi cha mabao 5-0.\
Pamoja na kushindwa kulipa kisasi, lakini Yanga imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi yoyote katika duru la pili na ndani ya mwaka 2013.
Katika tukio lililosisimua mashabiki waliokuwa uwanjani ki kitendo cha mwamuzi, Martin Saanya kuanguka wakati akienda kuwaamulia Kavumbangu na Nassoro Masoud 'Chollo' na kufanya pambano hilo kusimama kwa muda ili atibiwe na jingine ni lile la Ngassa kuvishwa jezi ya Yanga na kushangiliwa kwa kubebwa na wanachama wa Yanga walioimba karibu nyumbani.'
Katika mechi nyingine, Toto African na Polisi Moro licha ya kushinda mechi zao za nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting na Coastal Union, zimejikuta zikishuka daraja zikiungwana na African Lyon.
Toto iliifunga Ruvu mabao 2-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Polisi kuinyoa Coastal 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa mabao ya Kenneth Masumbuko na Ally Shomari.
Timu hizo zimeshuka daraja kwa vile Mgambo JKT ikiwa uwanja wa Mkwakwani ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lyon na kuvikisha pointi 28 ambazo zimeshindwa kufikiwa na Toto na Polisi ambazo zimemaliza na poinbti 25 tu.Nao Mtibwa Sugar imejikuta ikiloa mbele ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Chamazi, huku JKT Oljoro ilikubali kipogo cha bao 1-0 toka kwa Azam kwa bao la Seif Abdallah, na Kagera Sugar kuizamisha Prisons Mbeya kwa bao 1-0 kupitia kwa Paul Ngway alifunga dakika ya 87 katika lililofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya na kumaliza kwenye nafasi ya nne nyumba ya Simba.

Msimamo baada ya kumalizika kwa msimu wa 2012-2013:

                             P     W     D     L     F      A     D      Pts
Young Africans     26     18     6     2     47    14    33     60 
Azam                   26     16     6     4     46    20    26     54   
Simba                  26     12     9     5     39    26    13     45
Kagera Sugar       26     12     8     6     28     20     8     44    
Mtibwa Sugar      26     10     9     7      29     25    4     39  
Coastal Union     26      8     11      7     25     24    1     35   
Ruvu Shooting     26      8     7      11     23     28    -5    31    
JKT Oljoro FC   26      7     8      11     22     29    -7     29    
Tanzania Prisons  26      7     8     11     16     23     -7     29   
Ruvu Stars          26      8     5     13     22     39    -17     29
JKT Mgambo     26      8     4     14     17     27    -10     28
Toto Africans      26     5     10    11     24     33     -9     25
Polisi Morogoro  26     5     10    11     15     23     -8     25   
African Lyon       26     5     4     17     16     39     -23    19

No comments:

Post a Comment