Wachezaji wa Atletico Madrid wakitanua na taji lao la Mfalme |
Ronaldo alipomuumiza Gabi na kuzodolewa akitolewa uwanjani |
WALIOKUWA mabingwa wa Hispania, Real Madrid wamemaliza vibaya msimu wa 2012-2013 baada ya kubanjuliwa mabao 2-1 na wapinzani wao, Atletico Madrid katika Fainali ya Kombe la Mfalme, huku nyota wao Cristiano Ronaldo na kocha Jose Mourinho walilimwa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti.
Atletico waliokuwa kwenye uwanja wa ugenini wa wapinzani wao, Santiago Bernabeu walipata ushindi huo na kunyakua taji hilo katika muda wa nyongeza kwa mabao ya Diego Costa aliyefunga dakika ya 35 na lile la jioni la jioni la dakika ya 99 kupitia Joao Miranda lilitosha kuikata ngebe za Real waliotangulia kupata bao.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Ronaldo dakika ya 14 tu ya mchezo huo kabla ya kujikuta akiishia kutolewa nje na mwamuzi kwa kumpiga mchezaji wa Atletico, gabi kama ilivyokuwa kwa kocha wake ambaye ni mreno mwenzie, Mourinho maarufu kama 'the Only One' a.k.a Special One.
Kipigo hicho kimeifanya Real Madrid kumaliza msimu huu bila taji lolote kutokana nna ubingwa waliokuwa wanaushikili wa Ligi ya Hispania kunyakuliwa na watani zao Barcelona pia kuondolewa kwenye nusu fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment