STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 14, 2013

Imani za Kishirikina nusura livunje pambano la fainali 'mchangani'

wanaodaiwa watu wa 'kamati ya Ufundi' wakionyesha yao
Kikosi cha Manunda Fc
Kikosi cha G West walioibuka kidedea
PAMBANO la fainali la kugombea 'Kombe la Mbuzi' na Jezi kati Manunda Fc na G-West lililofanyika juzi kwenye uwanja wa Msisiri A, Mwananyamala nusura lishindwe kufanyika kutokana na vimbwanga vya vitu hizo kukataa katakata kubadili jezi zilizokuwa zikirandana kwa madai kwamba tayari zilishapitia kwa 'Babu'.

Licha ya jtihada ya mwamuzi na watu wenye ushawishi, kuzibembeleza timu hizo kukubaliana na pendekezo la waamuzi timu moja kubadili jezi, hakuna upande uliokubali na kumfanya mwamuzi kuafiki maamuzi ya timu hizo ili kuhofia kuvunja fainali hiyo iliyosisimua.

Pambano hilo liliishia kwa timu ya G West kuibuka mabingwa kwa njia ya mikwaju ya penati 4-2 baada ya dakika za kawaida matokeo yakiwa bao 1-1.

Wafungaji katika muda huo wa kawaida walikuwa Msimbe aliyeifungia Manunda kwenye dakika 43 na bao la kuwasawisha na wapinzani wao lilifungwa na Mome dakika 9 kabla ya mechi kumalizika.

Mbali na kimbwanga cha kugomea kubadilisha jezi hizo zilizofanana pambano hilo pia lilighubikwa na mambo ya kishirikina baada ya wachezaji wawili wa G-West kuanguka uwanjani kwa imani za kuzidiwa na majini, huku mashabiki kuvunja nazi na mayai kwa imani za ushirikina na wachezaji wa G-West kunyweshwa maji yaliyochanganywa na majani mithili ya Alovera badala ya maji ya kawaida na timu yao kuibuka mabingwa kwa mikwaju hiyo ya penati.
 

No comments:

Post a Comment