STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 14, 2013

Kaseba kuzipiga na Mmalawi, aahidi kushinda


BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa anayeshikilia taji la ubingwa wa taifa nchini, Japhet Kaseba anatarajiwa kupamba ulingoni mwezi ujao kuzipiga na Mmalawi Rasco Simwanza katika pambano la kimataifa la uzito wa kati.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) litakalosimamia pambano hilo, Emmanuel Mlundwa, mabondia hao  watapigana Juni 8 jijini Dar es Salaam na watasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia kadhaa.
Hilo litakuwa pambano la kwanza la kimataifa kwa Kaseba tangu aliporejea kwenye mchezo huo akitokea kwenye Kick Boxing ambapo aliwahi kutwaa ubingwa wa Dunia unaotambuliwa wa WCL na WKL.
Mlundwa alisema maandalizi yote ya pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Tan Academy, yanaendelea vyema na kwamba mashabiki wasubiri kupata burudani siku ya mpambano huo.
Mapambano ya utangulizi kwa siku hiyo itawakutanisha Juma Fundi dhidi ya Moro Best, Ibrahim Mahokola atakayepamba na  Kamanda wa Makamanda, Juma Seleman dhidi ya Issa Omar, na Ignas atakayeonyeshana kazi na Karega Suba.
Michezo mingine ni kati ya Jackie Hamis dhidi ya Kadani Chamwana, Aman Machuga dhidi ya Muhidini 'Ndolanga', Joseph Mbowe atakayepigana na Abdallah Mohammed na Kais Ramadhani atakayepepetana na Mikidadi Tyson.
Kaseba aliiambia MICHARAZO kwamba amejiandaa vyema kwa ajili ya pambano hilo kutokana na mazoezi anayoyafanya na kiu yake ya kutaka kujenga heshima katika ngumi kama alivyofanya kwenye Kick boxing.
"Nimeajiandaa vyema na kama nilipoahidi nilipotangaza kurejea kwenye ngumi naamini nitashinda pambano hilo na kuendelea kutamba ndani na nje ya nchi," alisema Kaseba anayefahamika zaidi kimichezo kama 'Champion'.

No comments:

Post a Comment