Kikosi cha Polisi Moro kinachopigana kuepuka kuteremka daraja |
African Lyon iliyokwishashuka daraja |
Kikosi cha Toto kilichovitani kuepuka kurudi 'mchangani' |
Mgambo JKT nayo ipo kwenye mtego wa kurudi FDL |
PAZIA la Ligi Kuu Tanzania bara linatarajiwa kufungwa rasmi siku ya Jumamosi kwa michezo saba tofauti, lakini ni mechi tatu tu kati ya hizo ndizo zitakazokuwa na mvuto na kufuatiliwa kwa karibu na mashabiki wa soka pengine kuliko hata pambano la watani wa jadi nchini, Simba na Yanga litakalochezwa Dar es Salaam.
Mechi hizo zitakazofuatiliwa kuliko la Simba na Yanga ambazo ni za kulinda heshima tu, ni ile ya jijini Mwanza kati ya wenyeji Toto Africans dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting, itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Hii ni kwa sababu Toto ipo katika janga la kushuka daraja na hivyo inahitaji ushindi huku ikiziombea Polisi Moro na Mgambo JKT ziteleze ili wenyewe waponee chupuchupu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Timu hiyo ina pointi 22 sawa na Polisi Moro na zinatofautiana idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa na iwapo itashinda itafikisha pointi 25 ambazo tatari zimeshafikiwa na Mgambo JKT iyakayokushuka dimbani nyumbani jijini Tanga kuumana na Africans Lyon iliyokwisha kushuka daraja.
Polisi Moro ambayo ilizinduka kwenye duru la pili ilipochukuliwa na kocha Mohammed Rishard 'Adolph' kabla ya kuzorota tena yenyewe itakuwa nyumbani kuumana na Coastal Union.
Kwa kulinganisha mechi hizo tatu za wawania kuepuka kushuka daraja unaweza kuona angalau Mgambo ipo katika nafasi nzuri ya kuokoka kuliko Toto na Polisi, hii ni kwa sababu inamaliza mechi za msimu na Lyon iliyoshuka daraja kitambo, huku ikisaka pointi moja tu kuwaokoa, ingawa kwa mechi mbili mfululizo timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu imeshindwa kuipata mbele ya Simba na Azam.
Pazia la ligi hiyo mbali na mechi hizo na ile ya watani wa jadi, pia litafungwa na mechi nyingine tatu ambapo JKT Ruvu dhidi ya Mtibwa Sugar, Prisons na Kagera Sugar na lile la washindi wa pili na wawakilishi wa Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili mwakani, Azam itakayokuwa ugenini mjini Arusha kuchuana na wenyeji wao JKT Oljoro.
P W D L F A D Pts
Young Africans 25 17 6 2 45 14 31 57
Azam 25 15 6 4 45 20 25 51
Simba 25 12 9 4 39 24 15 45
Kagera Sugar 25 11 8 6 27 20 7 41
Mtibwa Sugar 25 10 9 6 29 24 5 39
Coastal Union 25 8 11 6 25 22 3 35
Ruvu Shooting 25 8 7 10 23 26 -3 31
JKT Oljoro FC 25 7 8 10 22 28 -6 29
Tanzania Prisons 25 7 8 10 16 22 -6 29
Ruvu Stars 25 7 5 13 21 39 -18 26
JKT Mgambo 25 7 4 14 16 27 -11 25
Toto Africans 25 4 10 11 22 33 -11 22
Polisi Morogoro 25 4 10 11 13 23 -10 22
African Lyon 25 5 4 16 16 38 -22 19
Mechi za kufungia pazia msimu wa 2012-2013
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Toto African Vs Ruvu Shooting
Polisi Moro Vs Coastal Union
No comments:
Post a Comment