Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo (kushoto) akimkabidhi mmoja wa viongozi wa timu tatu walizozipa msaada wa fedha kushiriki vyerma katika RCL. Tukio ambaklo wadau wa soka wamelipongeza. |
WADAU wa soka mkoa wa Dar es Salaam wamekipongeza chama cha soka mkoa huo (DRFA) kwa kitendo chake cha kuzizawadia timu zake tatu zilizofuzu Ligi ya Mabingwa (RCL) wakidai ni kitendo kigeni kuwahi kufanywa na chama hicho kwa miaka mingi iliyopita.
Uongozi wa DRFA ulizipa fedha timu hizo wakiwamo mabingwa Red Coast, Abajalo na Friends Rangers kwa kufanya vyema kwenye Ligi Daraja la Pili, ili kuzisaidia kufanya vyema kwenye ushiriki wao wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa, iliyoanza juzi Jumapili.
DRFA iliwapa mabingwa wa mkoa huo Red Coast Sh. 700,000 na washindi wa pili Abajalo (Sh 600,000) huku walioshika nafasi ya tatu Friends Rangers wakiwapa Sh. 500,000.
Mmoja wa wadau walioipongeza DRFA kwa kitendo hicho ni Onesmo Waziri 'Ticotico' wa klabu ya Golden Bush FC, ambaye alisema kilichofanywa na uongozi mpya wa mkoa wao ni kigeni na kinachoonyesha uongozi huo ulivyo na dhati ya kuinua soka la mkoa huo.
Uongozi huo mpya wa DRFA uliingia madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufanyika uchaguzi mkuu uliomaliza miongo kadhaa ya utawala wa aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa chama hicho, Amin Bakhresa aliyeenguliwa mapema kwa kukosa sifa.
No comments:
Post a Comment