STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, May 8, 2013

Simba yaipumulia Azam, Chanongo apeleka furaha Msimbazi


Mfungaji wa bao pekee la Simba leo, Haruna Chanongo (kushoto)
BAO pekee lililotumbukizwa wavuni na mshambuliaji anayezidi kuja juu nchini, chipukizi Haruna Chanongo limeiwezesha Simba kuibuka kidedea mbele ya Mgambo JKT ya Tanga katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam jioni ya leo.
Ushindi huo ambao ni wa tatu mfululizo kwa Simba tangu walipojipanga upya wakizima 'mgogoro' uliokuwa ukifukuta chinichini klabuni kwao, imeifanya ifikishe pointi 45 na kutishia usalama wa Azam waliopo nafasi ya pili kwa muda mrefu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Azam ambayo imesaliwa na michezo miwili mkononi yenye ina pointi 48, tatu pungufu na ilizonazo Simba japo yenye imesaliwa na mechi mbili mkononi kabla ya kuhitimisha msimu wa 2012-2013.
Haruna Chanongo alifunga bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 8 tu ya mchezo huo baada ya kuwafungisha tela mabeki wa Mgambo kabla ya kufunga bao tamu lililoihakikishia Simba kukalia nafasi ya tatu na ikiinyemelea nafasi ya pili ya uwakilishi wa michuano ya kimataia mwakani iwapo itaifunga Yanga na Azam iteleze kwenye mechi zake ilizosaliwa nazo.
Kwa kipigo hicho cha leo, Mgambo imeendelea kupumulia mashine na kuziipa afueni Toto Africans na Polisi Moro katika hatari ya kushuka daraja, kwani maafande hao wanahitaji pointi moja tu kutoka baraka kwa wapinzani wao hao wawili waliopo nao mkiani kuteremka daraja wakiunga na Africana Lyon.
Timu hiyo itashuka dimbani Jumamosi jijini Dar es Salaam kuvaana na Azam katika mechi nyingine inayotabiwa kuwa ngumu kwao, ambako siku hiyo pia kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, wenyeji Kagera Sugar watawakaribisha Ruvu Shooting.
Katika pambano la leo vikosi vya timu hizo vilikuwa kama ifuatavyo:
Simba: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Miraji Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian, Amri Kiemba, Ramadhan Chanongo 'Messi' na Haruna Chanongo.
Mgambo JKT; Godson Mmassa, Salum Mlima, Ramadhan Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.

No comments:

Post a Comment