REDD'S MISS KIGAMBONI KWA MWAKA 2013 KUFANYIKA JUNI 7
Miss Kigamboni 2012, Eda
Sylvester (katikati) kushoto ni mshindi wa pili Agness Godluck (kulia)
ni mshindi wa tatu Elizabeth Boniface, walipotangazwa washindi mwaka
jana.
SHINDANO
la kumtafuta mrembo wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu "Redd's Miss
Kigamboni 2013" linatarajiwa kufanyika Ijumaa Juni 7 kwenye ukumbi wa
Navy Beach kuanzia saa 2:00 usiku hapa jijini Dar es Salaam.
Tayari
warembo wameshaanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na shindano hilo
ambapo wanajifua kwenye ukumbi wa Break Point (VIP) uliopo Posta hapa
jijini.
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya
shindano hilo yako katika hatua za mwisho na bado wanakaribisha warembo
wenye sifa za kushiriki shindano hilo kufika mazoezini kutoka sehemu
mbalimbali hapa nchini.
Mratibu huyo alisema kwamba
lengo la kuweka wazi na kuwahamasisha warembo ni kutaka kutoa nafasi kwa
wasichana wengi zaidi kujiandikisha na hatimaye kupata mshindi
atakayekiwakilisha vyema kitongoji hicho katika mashindano ya ngazi ya
Kanda yatakayofanyika baadaye mwezi ujao.
"Tumeshaanza maandalizi na
tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo wa hapa nchini kujiandaa kusubiri
Kigamboni kutoa mrembo wa taifa mwaka huu, tunawashiriki wenye mvuto na
sifa za ushindani," alisema Somoe.
Aliongeza kwamba fomu kwa
ajili ya kushiriki shindano hilo zinapatikana bure na warembo wanafanya
mazoezi chini ya Blessing Ngowi, ambaye mwaka juzi alishiriki fainali za
taifa za Redd's Miss Tanzania na alitwaa taji la Kanda ya Elimu ya Juu.
Alisema pia makampuni na
taasisi mbalimbali zinakaribishwa kudhamini shindano hilo ambalo mwaka
jana lilitoa mshindi katika kinyang'anyiro cha Kanda ya Temeke ambaye ni
Edda Sylivester.
Edda alifanikiwa kushika
nafasi ya tatu kwenye fainali za taifa huku mshindi wa taifa ni Brigitte
Alfred ambaye mwaka huu ataenda kupeperusha bendera ya nchi katika
mashindano ya dunia.
No comments:
Post a Comment