Sheikh Mkuu wa Tanzania, Muft Issa bin Shaaban Simba |
BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limelaani tukio la kulipuliwa kwa bomu kanisa la Katoliki mjini Arusha.
Jumapili iliyopita watu wasiojulikana walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu katika uzinduzi wa jengo la kanisa la la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kutokana na kitendo hicho BAKWATA kama chombo kikuu cha Waislam wametoa tamko lao juu ya tukio hilo kama inavyosomeka hapo chini. Tamko hilo lilitolewa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Sheikh Issa Bin Shaaban Simba.
TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA
Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.
Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini.

Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na
tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha
kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha
wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu
sote, Wakristo na Watanzania wote.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.
SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.

No comments:
Post a Comment