Na Boniface Wambura
PAMBANO namba 111 la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Simba
lililochezwa juzi (Mei 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
na kumalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1 limeingiza sh. 17,700,000.
Watazamaji
3,163 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 3,485,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 2,700,000.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 2,901 na kuingiza sh. 14,505,000 wakati idadi ndogo
ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki
28 na kuingiza sh. 560,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,772,416.50,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,063,449.90, Kamati ya Ligi
sh. 1,063,449.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
531,724.95, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
206,781.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
206,781.93.
Wakati huo huo Timu
za Simba na Mgambo Shooting ya Tanga zinaumana kesho (Mei 8 mwaka huu)
katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni vitakuwa sh. 5,000 kwa
viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000
kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 20,000.
No comments:
Post a Comment