Kesho ni Siku ya Mashujaa wa Tanzania waliokufa vitani kukumbukwa
KESHO ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania, ambapo kitaifa itafanyika mkoani Kagera, japo kila mkoa nao upo katika maandalizi ya kuadhimisha siku hiyo ya kuwakumbuka wale wote waliojitolea kupotea uhai wao kwa ajili ya taifa lao.
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwaongoza Watanzania katika maadhimisho hayo ya kesho.
Kwa mkoa wa Morogoro shughuli na maandalizi ya siku hiyo ziliendelea leo kama zinavyoonekana pichani ambapo hapo juu Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha maombolezi kikiwa katika mazoezi ya kutoa heshima za mwisho kwa mashujaa waliofariki dunia katika vita ya Kagera mwaka 1978 na 1979 wakati wa gwalide la pamoja la
jeshi la magereza, Polisi na JWTZ katika maandalizi ya mwisho ya kilele cha
maadhimisho ya siku kuwakubuka mashujaa hao ambayo yataadhimishwa kimkoa kwenye mnara wa kumbukumbu wa Posta julai 25 mkoani Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOG
Askari wa jeshi la polisi wakiwa katika gwalide
Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) nao wakiwa katika gwalide la pamoja.
Hapa ni askari wa jeshi la magereza wakiwajibika kwa ajili ya maandalizi hayo.
Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Mteule daraja la kwanza, Jonas Philipo kulia akitoa maelekezo eneo la barabara ya Stesheni.
Hapa Aande Philipo kulia akifafanua jambo kwa viongozi wakuu wa mkoa ndani ya jeshi na serikali.
Moshi ukiwa umezagaa baada ya kulipuliwa kwa mizinga mitatu katika maandalizi hayo.
Hapa
vikosi vyote vya JWTZ, Polisi na Magereza vikiingia katika eneo la
mzunguko wa posta ambapo ndiko kutaadhimishwa sherehe hizo kimkoa julai
25/ 2013.
No comments:
Post a Comment