KLABU ya Simba inapenda kutoa taarifa zifuatazo kwa umma
kupitia vyombo vyenu.
KUHUSU MCHEZAJI KIGGI
MAKASSY
UONGOZI wa Simba SC umefanikisha miadi (appointment) na
madaktari nchini India kwa ajili ya matibabu ya mchezaji wake, Kiggi Makassy.
Mchezaji huyo atakutana na madaktari nchini India Agosti 18
mwaka huu tayari kwa ajili ya kuanza matibabu ya matatizo yake ya goti
aliyoyapata wakati akiichezea Simba.
Ikumbukwe kwamba Simba SC ilikuwa klabu ya kwanza ya soka ya
Tanzania kupeleka mchezaji nchi za nje kutibiwa takribani miaka minne iliyopita
wakati ilipompeleka Uhuru Selemani Mwambungu nchini India.
Kwa taarifa hii, uongozi unapenda kuwahakikishia wapenzi na
wanachama wake kwamba dhamira ya klabu ni kuhakikisha wachezaji wanapewa
kipaumbele katika afya zao za kimwili na kiakili.
SIMBA DAY
Kama ilivyo ada, mwaka huu Simba itafanya maadhimisho ya
Siku ya Simba (SIMBA DAY). Siku hiyo itatanguliwa na WIKI YA SIMBA ambapo
wachezaji na viongozi wa klabu watatembelea vyombo vya habari, vituo vya
kulelea yatima na hospitali kwa ajili ya kutekeleza wajibu wake kwa jamii
(Social Responsibility).
MAANDALIZI YA LIGI
KUU
SIMBA imeingia kambini kwa ajili ya mazoezi makali
(intensive training) katika eneo la Bamba Beach jijini Dar es Salaam. Kocha
Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni, ameomba kambi hiyo ili kuwatengeneza
wachezaji kimwili, kiakili na kisaikolojia.
Kabla ya mechi ya Simba Day, timu itacheza mechi moja ya
kirafiki katika tarehe itayotangazwa baadaye.
Miongoni mwa wachezaji walio kambini ni Ramadhani Chomboh
(Redondo).
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
No comments:
Post a Comment