Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa, Taifa
Stars na benchi la ufundi wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Entebe nchini Uganda jana tayari kwa mchezo wa marudiano na timu ya Taifa ya
Uganda Jumamosi hii.
Timu
ya Taifa (Taifa Stars) imewasili Uganda jioni hii Jumatano tayari
kuikabili Uganda Cranes kwa mechi ya marudiano kutafuta tiketi ya
kucheza katika mashindano ya CHAN.
Kikosi
hicho chichi nye wachezaji 20, kiliwasili muda mfupi baada ya saa kumi
alasiri huku wachezaji na benchi la ufundi wakiwa na matumaini makubwa.
Akiongea
mara baada ya kuwasili Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen alisema
wamejiandaa vizuri wakiwa Mwanza na ana imanikikosi hiki kitabadili
atokeo ya awali ambapo Stars ilifungwa 1-0 na Cranes Jijini Dar es
Salaam.
Alisema
licha ya kuwakosa wachezaji Shomari kapombe na Mwinyi Kazimoto, ana
imani na kikosi chake hiki kuwa kitafanya makubwa Kampala.
“Tumekuja kubadilisha mahesabu kwani tumejiandaa vizuri kabisa,” alisema Poulsen.
Wadhamini
wa Stars, Kilimanjaro Premium Lager wamewaomba watanzania wasikate tama
kwani Stars bado ina nafasi kubwa ya kupindua meza.
“Sisi
kama wadhamini bado tuna imani na Stars na tunajua watatuwakilisha
vizuri ni vyema watanzania wawe na imani na kuiombea dua timu iibuke na
ushindi mnono katika mechi hii ya marudiano,” alisema Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, george Kavishe.
Mechi hii ni gumzo kubwa Jijini Kampala kwani baadhi ya waganda wana hofu kuwa henda wakafungwa nyumbani kwao.
Mechi hii itapigwa katika Uwanja wa Nambole Jijini Kampala JUmamosi hii saa kumi jioni.
Mashindano ya CHAN yanatarajiwa kufanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment