Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT, Dioniz Malinzi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mbio za Rocky Marathon.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu akifafanua jambo wakati
wa uzinduzi wa mbio za Rocky City Marathon uliofanyika jijini Dar es Salaam,
ambapo NSSF imedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleima Nyambui.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Rocky Marathon 2013 Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akizindua rasmi mbio za
Rocky City Marathon 2013 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Uhusiano
Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu
ambao wamedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15.
Picha ya pamoja.
MSIMU wa tano wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa, ambapo mdhamini mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
limetaka kuwepo kwa mgawanyo wa majukumu kwa mbio za umbali tofauti ili
kuharakisha uendelezaji wa vipaji vya wanariadha nchini.
Rock City Marathon zinaratibiwa na Kampuni ya Capital Plus
International (CPI), ambapo Ofisa Uhusiano wa NSSF inayodhamini mbio hizo kwa
mwaka wa nne sasa, Juma Kintu aliliomba Shirikisho la Riadha Tanzania RT
kugawana majukumu na wadau.
“Sisi kama NSSF tuko tayari kudhamini na kuchangia maendeleo
ya riadha nchini, ndio maana tunasisitiza mgao wa majukumu kwa wakimbiaji wa
umbali fulani kusimamiwa na taasisi au kampuni moja, ili kusaidia maendeleo ya
haraka na makuzi sahihi ya vipaji,” alisema Kintu.
Pamoja na NSSF, wadhamini wengine wa Rock City Marathon 2013
zitakazofanyika jijini Mwanza Oktoba 27 ni pamoja na PPF, Airtel, African
Barrick, Nyanza Bottlers, Sahara Media, Precission Air, Bank M, New Mwanza
Hotel na Umoja.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, aliyekuwa mgeni
rasmi, alisema mchezo wa riadha nchini unaelekea kuangamia na jitihada za
kuunusuru zinahitajika.
“Ni aibu kuwa mchezo wa riadha nchini unaelekea kufa wakati
viongozi waliopewa mamlaka ya kuhakikisha unaendelea wanashuhudia. Ni wakati wa
kuamka kuunusuru mchezo huu ambao katika miaka ya 1970 mpaka 1980 uliiletea
nchi yetu heshima kubwa.
Kwa upande wake, Rais wa RT, Suleiman Nyambui aliwataka
waratibu wa marathon kote chini kuhakikisha wanakuwa na mbio fupi za vijana ili
kupanua wigo wa kuzalisha vipaji vipya, vitakavyoliletea sifa taifa na kushinda
mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Naye Mgurugenzi Mtendaji wa Capital Plus, Ellen Otaru Okoedion,
aliishukuru Serikali kwa ahadi ya ushirikiano, lakini akaitaka kuhakikisha
inakaa mezani na (kina Nyambui) RT, ili kujadili njia sahihi zitakazofanikisha
kupatikana kwa kina ‘Nyambui wapya.’
Aidha, Mratibu wa tukio hilo, Mathew Kasonta alisema kuwa mbio
hizo zitajumuisha kilometa tano kwa
wakimbiaji kutoka katika makampuni, kilometa tatu kwa wenye ulemavu, kilometa
tatu kwa watu wazima (zaidi ya miaka 55) na kilometa mbili kwa watoto wenye
umri kati ya miaka 7 mpaka 10.
No comments:
Post a Comment