STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 20, 2013

Homa ya pambano la Man Utd, City yaanza

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01507/kompany_1507398a.jpg
Vincent Kompany
http://www.independent.co.uk/incoming/article8668976.ece/BINARY/original/wayne-rooney.jpg
Wayne Rooney


KATIKA kile kinachoonekena kama ni kuanza kupanda kwa 'homa ya pambano' baina ya wapinzani wa mji wa Manchester, Manchester United na Manchester City waachezaji wa timu hizo wameanza kutambiana.
Beki nmahiri wa Manchester City, Vincent Kompany amesema anasubiri kwa hamu kucheza dhidi ya Wayne Rooney keshokutwa Jumapili na anatumai kwamba mshambuliaji huyo wa Manchester United atakuwa katika kiwango chake cha juu.
Rooney amefunga magoli matatu katika mechi mbili tangu aliporejea katika kikosi kwa kwanza baada ya kupata jeraha la katika paji la uso lililomweka nje ya uwanja lakini nahodha huyo Man City alipuuza mitazamo kwamba anatamani kuona kiwango cha mshambuliaji huyo kinakuwa chini katika mechi yao ya mahasimu wa mji wa Manchester Jumapili.
"Hapana. Unahitaji kucheza dhidi ya wachezaji walio katika kiwango chao cha juu kabisa," aliwaambia waandishi wa habari. "Hivyo ndivyo ninavyoona. Daima nataka kucheza dhidi ya wachezaji wanaokuwa katika kiwango chao bora kabisa.
"Nina furaha sana kwa Wayne kwamba yuko katika kiwango cha juu. Huu ndiyo utamu wa Ligi kuu ya England, unacheza dhidi ya washambuliaji wakubwa wakati wote, lakini kuna wachezaji wengi wa kuchunga katika timu zote."
David Moyes na Manuel Pellegrini wanaelekea katika mechi yao ya kwanza ya watani wa jadi wa mji wa Manchester wakiwa kama makocha wa timu hizo, ingawa Mscotland huyo alishinda mechi nne mfululizo kwenye Uwanja wa Etihad baina ya mwaka 2008 na 2010 wakati akiifundisha Everton.
Lakini Kompany haamini kama matokeo hayo ya zamani yana mchango wowote katika kitakachotokea Jumapili.
"Ni timu tofauti, ni msimu tofauti na naweza kusema kwamba huwezi kutabiri matokeo ya mechi hii ya watani wa jadi," aliongeza. "Hakuna mtu aliyetabiri kwamba tungeshinda 6-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford (katika msimu wa 2011-12), kwamba wangetufunga kwenye Uwanja wa Etihad au kwamba tungeshinda Old Trafford (msimu uliopita). Nadhani hicho ndicho mashabiki wanachopenda. Mechi isiyotabirika.
"Ni mechi ambayo daima unaisubiri. Sidhani kama watu wa mjini Manchester tu bali duniani kote wanajiandaa kufurahia mechi hiyo.
"Ni mechi ambayo inavutia kwa mengi. Sijawahi kuichukulia poa na najiona kubarikiwa kucheza katika mechi hizo. Unafanya kila uwezalo kuhakikisha unacheza vyema katika mechi hizi."
 





No comments:

Post a Comment