Kamanda Suleiman Kova |
JESHI la Polisi Jijini Dar es Salaam limeyapiga marufuku maandamano ya umoja wa
vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA yaliyopangwa kufanyika kesho Jumamosi.
Maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa
kuanzia Tazara hadi Jangwani kisha Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali .
Taarifa iliyotolewa na Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova kupitia ITV imeeleza kuwa Polisi wamechunguza na kugundua kwamba maandamano hayo yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano.

No comments:
Post a Comment