STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 20, 2013

Shafii Dauda achimba mkwara mzito, kisa...!

Shafii Dauda
MCHAMBUZI maarufu wa soka nchini, Shafii Dauda ameuchimba mkwara uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaodaiwa kutaka kuendelea kumwekea mizengwe katika kuwania uongozi ndani ya shirikisho hilo.
Dauda, ambaye ni miongoni mwa wagombea waliokuwa wameondolewa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF utakaofanyika mwezi ujao na kurudishwa na kamati ya Maadili ametema cheche hizo kupitia akaunti ya Facebook.
Mwanamichezo na mtangazaji huyo, amelazimika kuchimba mkwara huo baada ya kusisikia fununu za kutaka kuwekewa zengwe kama ilivyowahi kusikia awali na kujikuta kweli jina lake likitupwa kwa madai ambayo hayakuonekana kama ana hatia.
Dauda ameomba kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ambapo jina lake la wenzake kadhaa yalitemwa kabla ya Kamati ya Maadili ya TFF chini ya Jaji Jesse Mguto kuwarejesha tena kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27.
Ebu isome mwenyewe ujumbe huo, ingawa kuna baadhi ya sarufi tumezirekebisha ili ziende sawia la lugha fasaha ya kiswahili;
"Siku chache za nyuma nilizisikia njama za baadhi ya viongozi wa TFF kutaka kuondoa jina langu kwenye mchakato wa uchaguzi wa TFF na kulipeleka kwenye kamati ya Maadili eti nili-publish barua ya FIFA kwenye blog yangu bila idhini yao, nikazipuuzia nikidhani ni stori tu za mitaani,muda ulipofika Taarifa ya TFF ikatoka kweli jina langu likapelekwa kwenye kamati ya Maadili kwasababu zile zile nilizozisikia kabla kwa watu,Kamati ya MAADILI ikaniita nikayasikiliza mashitaka ya Secretarieti ya TFF ambayo iliwakilishwa na Afisa Habari ndugu yangu Boniface Wambura ikanihoji namimi nikatoa utetezi wangu na hatimaye kamati ikaonelea sina kesi ya kujibu hivyo basi jina langu likarudishwa kwenye mchakato wa uchaguzi. Kutoka kwenye vyanzo vyangu mbali mbali ndani ya TFF eti sasa wanajipanga kesho kutoa PRESS ya kuliondoa tena jina langu eti kwa kigezo sina UZOEFU,sasa ninachowambia kama ni kweli yanayozungumzwa WASITHUBUTU kufanya hivyo kwani kwa mara nyingine tena watanipa pointi 3 za mezani.IJUMAA KAREEM!

No comments:

Post a Comment