HATA hivyo wakati BAKWATA wakitoa taarifa hiyo ni kwamba kwa wale wanaofuata mwezi muandamo wa kimataifa ni kwamba Waislam watafunga Arafah kuwaunga mkono mahujaji siku ya Jumatatu na kuisherehekea sikukuu Jumanne itakayokuwa Oktoba 15, yaani siku moja kabla ya ile iliyotangazwa na BAKWATA.
Funga ya Arafah ni muhimu kwa waumini wa kiislam ambao hawakubahatika kwenda Hijja kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) kufunga Swawm siku ya
'Arafah kwa sababu ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili; mwaka uliopita
na baada yake (Hadiyth katika Swahiyh Muslim).
Hivyo MICHARAZO inawakumbusha waumini wa dini hiyo kutoisahau swaumu hiyo, japo tumesisitizwa kufunga tangu Mfungo tatu unapoingia katika makundi ya mwanzoni, lakini kwa wale walioshindwa kutekeleza ibada hiyo shime wasiiache Arafah kwa manufaa yao ya kidunia na Ahera Inshallah
No comments:
Post a Comment