Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,(kulia) akisisitiza jambo katika mkutano wake leo na wanahabari kuhusu ujio wa P Square. Kushoto ni Mtangazaji, Hillary Daud 'Zembwela'. |
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, mtangazaji wa kituo hicho, Hillary Daudi maarufu kama Zembwela alisema show hiyo itakuwa ya aina yake.
“Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema.
“Hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa Bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi.”Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema Vodacom inafurahi kuendelea kuwa sehemu ya kutoa burudani kwa jamii ya Watanzania na safari hii ikiwaleta wasanii ambao ni kipenzi cha Watanzania wengi.
“Siku zote Vodacom imeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa Watanzania, kuanzia katika burudani na hata huduma nyingine za mawasiliano na kijamii. Tunaendelea kuunga jitihada za kuwainua wasanii wetu wa ndani kwa kuwapatia fursa ya kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao wakubwa waliofanyikiwa kufanya kazi zao Kimataifa,” alisema.
“Kwa wateja wa Vodacom ambao pia ni mashabiki wa wasanii hawa ambao wanatamba na kibao chao kitamu cha ‘Personally’ kwa sasa wanayo fursa ya kufurahia nyimbo hizi kwa kuzidownload au kuzitumia kama miito ya simu (RBT) na kuweza kujishindia tiketi za onesho hilo. Natoa wito kwa Watanzania wapenda burudani kutembelea ukurasa wetu wa Facebook na Twitter kwa taarifa zaidi na kujua namna ya kujishindia tiketi za onesho hilo.”
No comments:
Post a Comment