Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliyewatoa kifungoni waliokuwa wamefungiwa katika soka |
Oktoba 28 mwaka huu wakati
akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF,
Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa sababu
mbalimbali.
Hata hivyo, msamaha huo
hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa au kupanga matokeo.
Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.
Vyama
vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao
(vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote
waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).
No comments:
Post a Comment