STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Everton yaua ugenini, Chelsea ikiifuata Arsenal Emirates leo

Everton wakishangiulia bao lao la ushindi jana usiku mbele ya Swansea City
WAKATI Everton wakipata ushindi muhimu jana ugenini dhidi ya Swansea City, Arsenal na Chelsea leo zitakuwa kibaruani kutaka kurejea kwenye nafasi zao ilizokuwa ikizishikilia awali.
Arsena ilienguliwa kileleni na kuporomoshwa hadi nafasi ya tatu katika msimamo itakuwa nyumbani kuikaribisha Chelsea iliyoshushwa jana hadi nafasi ya tano baada ya Everton kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Swansea City.
Timu hizo mbili zinakutana zote zikitokea kupoteza mechi zao za mwisho, Arsena ikipoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Napoli katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manachester City waliowasulubu kwa mabao 6-3.
Chelsea wenyewe walitoka kupokea kipigo cha aibu cha mabao 2-1 toka kwa vibonde wa Ligi Kuu, Sunderland katika mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One), huku ikishuhudiwa mabao yote matatu ya mchezo huo yakifungwa na vibonde hao na kutinga Nusu Fainali.
Ushidni wowote kwa timu hizo utakuwa na maana ya kurejea kwenye nafasi zao za awali, Arsena kurejea kileleni kunakoshikiliwa kwa sasa na Liverpool na Chelsea yenye pointi 33 ikishinda itakwea nafasi ya pili nyuma ya Liverpool wenye pointi 36 kwa sasa baada ya Jumamosi kushinda mabao 3-1 dhidi ya Cardiff City.
Arsena yenyewe ikishinda itafikisha jumla ya pointi 38 na kuziporomosha Liverpool; Manchester City inayokamata kwa sasa nafasi ya pili na hivyo itashuka dimbani katika pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Micheal Dean ikiwa na usongo wa kuizuia Chelsea ambayo katika mechi tatu mfululizo zilizopita baina yao wamekuwa wanyonge kwa kufungwa zote.
Katika mechi ya jana usiku, Swansea ikiwa nyumbani ilishindwa kuhimili vishindo vya wageni wao Everton ambao walifunga mabao yote matatu yaliyopataikana jana yakiwemo mawili yao ya ushindi na lile la kufutia machozi la wenyeji hao.
Everton waliandikisha bao la kwanza dakika ya 66 kupitia kwa Seamus Coleman kabla ya Bryan Oviedo kujifunga dakika nne baadaye na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Hata hivyo alikuwa ni Ross Barkley aliyeihakikishia wageni ushindi kwa kufunga bao dakika sita kabla ya pambano hilo kumalizika kwa mkwaju wa frikiki na kuifanya Everton kufikisha pointi  34 na kushika nafasi ya nne nyuma ya Arsenal yenye pointi 35.

No comments:

Post a Comment