STRIKA
USILIKOSE
Monday, December 23, 2013
Japhet Kaseba atetea taji lake la PST kwa KO
Pambano hilo lililoandaliwa na Bigright Promotions na kusimamiwa na PST na lililotanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizzi lilifanyika kwenye ukumbi wa Friends Corner Manzese, jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo wa Kaseba umemfanya aendeleze rekodi yake nzuri ya kushinda mfululizo nyumbani tangu arejee katika ngumi akitokea kwenye kickboxing, alikokuwa bingwa dunia wa WKL na WKC.
Katika pambano hilo lililokuwa la raundi 10, Kaseba alimuendesha puta mpinzani wake kwa muda mrefu wa pambano hilo kabla ya Alibaba kusalimu amri raundi ya nne na kumfanya Kaseba kusherehekea ubingwa akiufunga mwaka 2013.
Kaseba alitwaa taji hilo kwa kumchakaza Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' mara mbili mfululizo mwishoni mwa mwaka juzi na mapema mwaka huu kabla ya kumchaka Mmalawi Pascal Simwanza kwa TKO Juni mwaka huu.
Hata hivyo hivi karibuni mkali huyo aliingia kwenye orodha ya mabondia wa Tanzania wasioweza kutamba nje ya nchi baada ya kwenda kupigwa kwa KO ya raundi ya 2 nchini Australia dhidi ya mwenyeji wake Jeremy Van Diemen.
Katika michezo mingine ya utangulizi katika ukumbi huo, mkali wa kickboxing mtanzania anayeishi Canada, Kareem Kutch alinshinda kwa pointi Omar Juma 'Tata Boy', huku Omar Nampekecha 'Peche Boy'; akishinda pia kwa pointi dhidi ya Hassani Kiwale.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment