Mario Balotelli akikosa bao la wazi langoni mwa Inter Milan |
'Muuaji; akishangilia bao lake |
Licha ya kipigo hicho pia, Milan ilipata pigo dakika za lala salama wakati kiungo wake, Sulley Muntari alipolimwa kadi nyekundu wakati mchezo ukielekea kumalizika.
Palacio raia wa Argentina aliifungia Inter bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Fredy Guarin na kuzidi kuicha Milan izidi kuchechemea kwenye ligi hiyo ikishika nafasi ya 13, huku wapinzani wao kwa ushindi huo wamekwea hadi nafasi ya tano ikifikisha pointi 31.
Kipigo hicho kimekuja baada ya Milan kupata sare mfululizo katika mechi zake za hivi karibuni katika ligi na kuliacha benchi la ufundi la mabingwa hao wa zamani wa Ulaya wakiweweseka kujiweka sawa kabla ya kuwakuta yaliyowakuta makocha wa klabu nyingine waliotimuliwa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Livorno ililala nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Udinese, Cagliari ililazlimishwa sare ya 1-1 na Napoli kwa mechi zilizochezwa Jumamosi.
Mechi zilizochezwa jana Bologna ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa, Atlanta ikalala kwa mabao 4-1 nyumbani kwake mbele ya mabingwa watetezi Juventus, huku Hellas Verona ikiishindilia Lazio kwa mabao 4-1.
Nayo Roma iliendeleza mauaji kwa kuilaza Catania kwa mabao 4-0, Sampodoria na Parma zikitoka sare ya 1-1 na Fiorentina ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Sassuolo na Chievo Verona ikilala ugeninikjwa mabao 4-1 toka kwa Torino.
No comments:
Post a Comment