STRIKA
USILIKOSE
Monday, December 23, 2013
Maskini Cheka! Apigwa kwa KO Russia, Kamote naye hoi
MKALI wa ngumi za kulipwa na bingwa wa dunia wa WBF, Francis Cheka ameendelea kuwa 'urojo' akicheza nje ya ardhi ya Tanzania baada ya mwishoni mwa wiki kuchezea kipigo cha KO ya raundi ya tatu akiwa nchini Russia.
Cheka anayeshikilia mikanda mingine kadhaa ukiwemo wa IBF Afrika, UBO na ICB, hajawahi kushinda pambano hata moja nje ya Tanzania, ingawa ana rekodi nzuri ya kushinda mfululizo akiwa nyumbani tangu mwaka 2008.
Bingwa huyo alikuwa nchini Russia kupigana na mwenyeji wake, Fedor Chidinov ambaye anashikilia rekodi ya kucheza mapambano 9 bila kupoteza wala kutoka sare mchezo wowote.
Pambano hilo lilichezwa kwenye ukumbi wa Dynamo Palace of Sports katika mji wa Krylatskoye jijini Moscow likiwa ni pambano la kwanza kwa Cheka tangu atwae taji hilo la WBF kwa kumpiga Mmarekani Phil Williams Agosti 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Pia lilikuwa ni pambano la sita mfululizo kwa Cheka anayesifiwa kuwa na pumzi na ngumi kali kupoteza nje ya nchi tangu mwaka 2008.
Katika pambano hilo la Jumamosi, Cheka alishindwa kuhimili makonde ya mpinzani wake katika pambano hilo la uzito wa Super Middle lililokuwa la raundi nane na kuishia raundi ya tatu.
Naye bongwa wa kimataifa wa WB-Forum, Allen Kamote aliyeambatana na Cheka nchini Russia aliangukia pua kwa kupigwa TKO ya raundi ya pili na Eduard Troyanovsky katika pambano hilo la uzito wa Light lililokuwa la raundi kumi lililochezwa kwenye ukumbi huo huo.
Kamote anayetokea Tanga ilibidi aokolewe na mwamuzi wa mpambano huo ili isizimishwe kabisa na mpizani wake anayeshiukilia rekodi ya kucheza mapambano 17 bila kupigwa wala kutoka sare na akishikilia nafasi ya pili nchini mwake katika uzito huo.
Huenda kipigo cha Kamote kimetokana na uchovu kwani ni wiki mbili tu zilizopita alicheza pambano lake la mwisho dhidi ya Deo Samuel na kushinda kwa pointi katika shamrashamra za sherehe za siku ya Uhuru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
sijui tatizo n nini kwa cheka. Fuatilia huo mpambano hapo chini jinsi cheka alivyopelekeshwa mpaka aibu kuamini km ni kweli bingwa wa dunia. Nadhani umefika wakati mapropmota kutuletea mabondia wa ukweli kutoka nje na cyo wababaishaji.
ReplyDeletehttp://translate.google.co.tz/translate?hl=en&sl=ru&u=http://www.youtube.com/embed/rkb-EdcpqsQ%3Fwmode%3Dtransparent&prev=/search%3Fq%3DFrancis%2BCheka%26sa%3DX%26biw%3D1366%26bih%3D643%26tbs%3Dqdr:d
http://translate.google.co.tz/translate?hl=en&sl=ru&u=http://www.youtube.com/embed/rkb-EdcpqsQ%3Fwmode%3Dtransparent&prev=/search%3Fq%3DFrancis%2BCheka%26sa%3DX%26biw%3D1366%26bih%3D643%26tbs%3Dqdr:d
ReplyDelete