Baadhi ya viongozi wa sasa wa TBF katika mikutano yao na wanahabari |
Uchaguzi huo utakwenda sambamba na mkutano mkuu wa shirikisho hilo ambao utafanyika siku moja kabla huku ukihudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa TBF, Mussa Mziya, ilieleza tarehe hiyo imetangazwa baada ya wajumbe kuridhia na kukubaliana.
Aliema kutokana na ukata unaolikabili shirikisho hilo, wamewaomba wajumbe wote wa mikutano wajigharamie kwa nauli, malazi na chakula kwa kipindi chote cha mkutano na uchaguzi.
Rais huyo aliwataka wadau na makampuni mbalimbali kujitokeza ili kuwadhamini na kwamba fedha zinazohitajika kwa ajili ya gharama za uchaguzi huo ni Sh. milioni 17.
Alisema ada za fomu kwa wanaotaka kugombe nafasi ya urais na makamu wa rais ni Sh. 150,000, nafasi ya katibu mkuu, katibu mkuu msaidizi na mweka hazina ni Sh. 100,000. Kwa upande wa wajumbe wa kamisheni zote ni alisema ni Sh. 50,000 huku mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za ikiwa ni Desemba 13, 2013 saa tisa mchana.
Awali uchaguzi huo uilitangazwa kufanyika Mbeya Desemba 10 siku moja baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Taifa kwa mchezo huo ambao kwa sasa limeota mbawa kufanyika kwake.
No comments:
Post a Comment