STRIKA
USILIKOSE
Thursday, January 30, 2014
City yafanya 'mauaji' ikikwea kileleni, Chelsea yabanwa 'darajani'
MANCHESTER City wakiwa kwenye kiwango bora kabisa kwa sasa usiku wa jana iliisasambua Tottenham Hotspur kwao kwa kuibugiza mabao 5-1 katia mechi ya Ligi Kuu ya England na kukwea kileleni ikiiondosha Arsenal.
Mabao ya Sergio 'kun' Aguero, mkwaju wa penati wa Yaya Toure uliotokana na madhambi yaliyofanywa na beki Danny Rose na mengi ya Edin Dzeko, Jovetic na Vincent Kompany yalitosha kuifanya City kuendelea kushinda mfululizo kwa idadi kubwa ya mabao na kukalia kiti cha uongozi ikiwa na pointi 53, moja zaidi ya Arsenal waliolazimishwa sare ya 2-2 juzi juzi na Southampton ikiwa ugenini.
Wenyeji waliomaliza wakiwa pungufu baada ya Rose kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 50 ilipata bao lake la kufuitia machozi dakika ya 59 kupitia kwa Etienne Copoue.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa jana, Chelsea wakiwa nyumbani kwao kwenye uwanja wa Stanford Bridge walilazimishwa suluhu ya bila kufungana na West Ham United, huku Sunderland wakizidi kufufuka kwa kuichapa Stoke City kwa bao 1-0 na Aston Villa wakiwa nyumbani kwao wakipata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya West Bromwich.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment