STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 9, 2014

AC Milan Mwaka wa Majanga, Napoli yainyoa 3-1

Adel Taarabt akiifungia Milan bao la mapema
MWAKA wa tabu umeendelea kuiandama timu ya AC Milan baada ya usiku wa kuamkia leo kupokea kipigo cha mabao 3-1 ikiwa ugenini dhidi ya Napoli na kuzidi kuiweka pabaya mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.
Milan ambayo kwa sasa inanolewa na kocha Clerence Seedorf, imekuwa na mwenendo wa kusuasua katika Ligi Kuu ya Italia (Seria A) ndani ya msimu huu ambapo kwa kipigo cha jana kiliwaacha kwenye nafasi yao ya 10 ikiwa na pointi 29 ambapo ni 30 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Juventus wenye pointi 59 na mchezo mmoja mkononi.
Wageni ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 8 lililofungwa na mchezaji mpya aliyesajiliwa toka Fulham ya  Uingereza, Adel Taarabt kabla ya  Gökhan  Ä°nler kuisawazishia Napoli dakika tatu baadaye akimalizia kazi nzuri ya Jorginho.
Matokeo hayo yalisalia hadi timu hizo zilipoenda mapumziko kabla ya wenyeji kuanza kwa kasi kipindi cha pili na kujipatia bao la pili lililowekwa kimiani na Muargentina, Gonzalo Higuain dakika ya 56 akimaliza kazi ya Inler.
Higuain aliihakikishia Napoli ushindi mnono nyumbani kwa kuifungia bao la tatu dakika ya  82 akimalizia pasi ya José Callejón.
Matokeo hayo ameifanya Napoli kujikita katika nafasi ya tatu mbele ya Fiorentina kwa kufikisha pointi 47.
Fiorentina imefikisha pointi 44 baada ya mapema jana kupata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Atalant, huku Udinese ikishinda pia nyumbani kwa kuilaza Chievo mabao 3-0.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezpo kadhaa Torino  itaumana na Bologna,    Sampdoria itapepena na Cagliari, Parma itaialika Catania, Livorno itaumana na Genoa,
Hellas Verona itakwaruzana na vinara wa ligi hiyo Juventus, Lazio itaikaribisha Roma na Inter Milan itaumana na Sassuolo.

No comments:

Post a Comment