Gareth Bale akifunga bao la kwanza la Madrid ikiwa nyumbani jana |
Pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, wenyeji Madrid walianza mapema kuonyesha dhamira yao ya kupata ushindi kwa kuandika bao la kwanza lililofungwa na Gareth Bale katika dakikia ya 7 tu ya mchezo.
Mfaransa Karim Benzema aliiongezea Madrid bao la pili dakika ya 25 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Bale na dakika mbili kabla ya mapumziko, Mario aliifungia wageni bao la kufutia machozi.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana na kufanya mabadiliko kadhaa yaliyozisaidia timu hizo, japo wenyeji walinufaika zaidi kwa kuongeza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Jesé RodrÃguez dakika ya 64 baada ya kazi nzuri ya Angel di Maria na Benzema kuongeza jingine dakika ya 76 japo wageni alitangulia kupata bao lao la pili la kufutia machozi lililowekwa kimiani na Giovan dos Santos dakika ya 69.
Ushindi huo umeifanya Madrid kufikisha pointi 57 sawa na Atletico Madrid ambayo yenyewe iulinyukwa ugenini mabapo 2-0 na Almeria na kumpoteza kipa wake aliyeoonyeshwa kadi nyekundu.
Katika mechi nyingine za ligi juzi Espanyol ilishinda bao 1-0 nyubani dhidi ya Granada huku Valencia jana iliishindilia bila huruma Real Betis kwa mabao 5-0 na Rayo Vallecano kuichapa Malaga mabao 4-1.
Leo kutakuwa na mechi nyingine kadhaa ya ligi hiyo ambapo Osasuna itaumana na Getafe, Real Valladolid kuvaana na Elche, huku Real Sociedad itaonyeshana kazi na Levante, Sevilla itaikaribisha mabingwa watetezi Barcelona na keshokutwa Celta Vigo itaialika Athletic Club nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment