Darren Bent akiisawazishia Fulham bao dakika za lala salama |
Manchester United walioonekana kama wamevuna pointo zote tatu baada ya Robin van Persie na Michael Carrick kufunga mabao mawili na kuinyamazisha Fulham waliotangulia kupata bao la mapema la dakika 19 lililofngwa na Steve Sidwell.
Juan Mata alimtengenezea nafasi nzuri van Persie aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya 78 kabla ya Carrick kuongeza la pili dakika mbili baadaye.
Hata hivyo mashabiki wa Old Trafford wakiamini wapata ushindi nyumbani, Bent alifunga bao la kusawazisha dakika nne za nyongeza za mchezo huo na kuipa pointi moja Fulham ugenini.
Matokeo hayo yameendelea kuiacha Manchester ambayo Jumatano itaifuata Arsenal iliyonyukwa jana na Liverpool kwa mabao 5-1, ikibaki nafasi ya saba ikiwa na pointi 41.
No comments:
Post a Comment