NAPE NNAUYE |
DAR ES SALAAM, Tanzania
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na
kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani
uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23.
Akitoa
shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema
leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia
wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba
hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Akizungumzia
kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga
watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa
na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA
wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na
utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba
Watanzania hawakiamini," alisema.
Katika
uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za
Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage
(Shinyanga), Ibumu na Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga),
Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti
(Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).
No comments:
Post a Comment