STRIKA
USILIKOSE
Monday, February 10, 2014
Twiga Stars kuagwa Jumatano
TIMU
ya Twiga Stars itaagwa rasmi Jumatano (Februari 12 mwaka huu) tayari
kwa safari ya Lusaka, Zambia kwa ajili ya mechi ya kwanza ya raundi ya
pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) ambayo fainali zake
zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia. Msafara wa timu hiyo
itakayoondoka kwa ndege ya Fastjet utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd
Mgoyi.
Hafla
ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi
za TFF. Timu hiyo itaondoka Februari 13 mwaka huu alfajiri tayari kwa
mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment