Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo ya
msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika
Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72) aliyefariki dunia
usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa
hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI) jijini Dar es
Salaam.
Marehemu
Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi kushika
nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika na
baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa akisumbuliwa
na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa kulikosababishwa na
hitilafu ya figo.Kwa
mujibu wa msemaji wa familia, Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa
kuagwa rasmi kesho kabla ya kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha
Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha Qorro na
wanafamilia wengine nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa
Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)
aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda
mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (
MOI) jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment