Timu
ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo) inatua nchini kesho mchana (Februari
27 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa
Wanawake (AWC) dhidi ya Tanzania (Twiga Stars) itakayochezwa keshokutwa
(Februari 28 mwaka huu).
Shepolopolo
yenye msafara wa watu 29 itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka
na itafikia kwenye hoteli ya Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo
itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi kuanzia saa 10
kamili jioni.
Waamuzi
wa mechi hiyo kutoka Burundi wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili
nchini leo asubuhi wakati Kamishna Fran Hilton-Smith kutoka Afrika
Kusini atawasili kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa
ndege ya South African Airways.
Katika hatua nyingine Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa
na mkutano na waandishi wa habari juu ya benchi la ufundi la timu ya
Taifa ya wakubwa (Taifa Stars).
Mkutano
huo utafanyika kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi
za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden
na Ohio.
No comments:
Post a Comment