Manchester Utd walipokuwa wakihenyeshwa uwanjani jana |
Wachezaji wa Manchester United wakiwa hawaamini kilichjowakuta Ugiriki jana |
Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Mashetani Wekundu kwa timu hiyo ya Ugiriki katika miaka minne iliyopita kwani Olympiacous ilikuwa haijawahi kuifunga Manchester Utd katika michuano ya kimataifa.
Vijana wa David Moyes, walishindwa kuhimili vishindo vya vinara hao wa Ligi Kuu ya Ugiriki, kwa kufungwa mabao hayo moja kila kipindi na kupata kibarua kigumu cha kushinda nyumbani kwao kwa mabao 3-0.
Mabao yaliyoiangamiza Manchester Utd na kutimiza tambo za kocha wa timu hiyo ya Ugiriki kwamba wangeshinda mchezo huo, yalifungwa na Alejandro Dominguez aliyefunga dakika ya 38 kabla ya nyota wa Arsenal anayecheza kwa mkopo Olympiacos, Joel Campbell kumaliza udhia katika dakika ya 55.
Kipigo cha Mashetani Wekundu imekuwa kama muendelezo wa aibu kwa timu za England katika hatua hiyo ya 16 baada ya wiki iliyopita Arsenal na Manchester City kufungwa idadi kama hiyo nyumbani na timu za Bayern Munich na Barcelona.
Timu nyingine ya England Chelsea leo itajaribu bahati yake kwa kuvaana na Galatasaray uwanja wa ugenini nchini Uturuki, huku mechi nyingine ya leo ni ile ya Schalke 04 itakayoikaribisha Real Madrid.
Katika mechi nyingine ya mapema jana, wenyeji Zenit ya Urusi ilifumuliwa mabao 4-2 na wanafainali wa mwaka jana Borussia Dotmund ya Ujerumani ambapo hadi mapumziko walikuwa nyuma 2-0.
Mabao yaliyoiweka Dotmund katika nafasi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya mwaka huu yalifungwa na Mkhitaryan, Reus kabla ya Robert Lewandowski kufunga mawili na wenyeji yaliwekwa kimiani na Shatov na Hulk.
No comments:
Post a Comment