SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya
mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors)
itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia, ndani yake
wakiwemo wachezaji sita wa Yanga SC.
Hata hivyo kipa tegemeo na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Juma Kaseja akiwa ameachwa nje.
Kikosi hicho kilichotangazwa na TFF badala ya kocha mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen na kuashiria kupewa 'mkono wa kwaheri' kwa kocha huyo kutoka Denmark na kitakachoingia kambini Machi Mosi na kuondoka nchini Machi 3 kwenda kuivaa wenyeji wao ni pamoja na makipa watatu ambao ni Deogratius Munishi (Yanga),
Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam).
Wengine waliotajwa ni mabeki wa pembeni ni Edward
Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City)
na Michael Aidan (Ruvu Shooting).
Mabeki
wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga),
Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya
Sports Club, Qatar).
Washambuliaji
ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis
Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini
Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka
Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.
TFF
imesema wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya
kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi
zao kumalizika.
No comments:
Post a Comment