STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Noma! Raia wa UK agundulika kuambulizwa Ebola


Daktari wa Ebola nchini Liberia
Raia mmoja wa Uingereza anayeishi nchini Sierra leone ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Idara ya afya imethibitisha kisa hicho.
Tangu mwezi machi zaidi ya watu 1400 wameripotiwa kufariki magharibi mwa Afrika.
Idara ya afya imesema kuwa raia wa kwanza mwingereza kuambukizwa ugonjwa huo alikuwa anaishi Sierra Leone.
Taifa hilo ni miongoni mwa mataifa ambayo yameathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Mwathiriwa wa Ebola aliyepona
Iwapo atapewa matibabu nchini Uingereza mgonjwa huyo ana uwezekano mkubwa wa kupata nafuu kwa sababu hospitali za Sierra Leone zimejaa waathiriwa wa ugonjwa huo hatari ambao unaendelea kuenea kwa kasi.
Eneo la kuwatenga wagonjwa tayari limebuniwa katika hospitali ya Royal free mjini London.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa ebola,ijapokuwa dawa ya majaribio iliwasaidia raia wawili wa Marekani kupona huku maafisa watatu wa afya pia wakionyesha dalili za kupata nafuu walipoitumia dawa hiyo nchini Liberia.
Katika mataifa ya afrika magharibi wakaazi wengi wamekuwa wakiogopa kuwatoa ndugu zao wanaoathiriwa na ebola kwa hofu ya kutowaona tena.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment