STRIKA
USILIKOSE
Sunday, August 24, 2014
UDA kununua dalada zote Dar...Kivipi?
Na Suleiman Msuya
SHIRIKA la Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam (UDA) kupitia bodi ya wakurugenzi limesema lipo tayari kuwalipa au kununua hisa za wasafirishaji watakao kuwa wapo tayari wakati wa mradi wa mabasi yaendayo kasi utakapoanza katika barabara ya Morogoro.
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Kamati Maalumu ya Umoja wa Wamiliki wa mabasi ya usafiri Mkoa wa Dar esSalaam UWAMADA Therese Kitambi wakati akitoa taarifa kwa wajumbe kwenye mkotano uliofanyika kwenye ukumbi wa Kareemjee jijini Dar es Salaam.
Alisema katika mazungumzo ambayo wameyafanya walifikia muafaka kuwa UDA wapo tayari kununua mabasi ya wale wamiliki ambao watakuwa hawapo tayari kuwa na hisa katika kampuni hiyo na kwa wale ambao watakuwa tayari wataruhusiwa kununua hisa.
Kitambi alisema makubaliano hayo ni ya awamu ya kwanza ya mradi wa barabara ya Morogoro na hayahusi awamu zote za mradi huo wa mabasi yaendao kasi ambao utahusu takribani barabara zinazoingia mjini.
“Ndugu zangu wajumbe napenda kuwatarifu kuwa UDA wapo tayari kuungana na sisi kwa Yule ambaye atakuwa tayari ila kama hutaki anaweza kununua gari lako kulingana na thamani yake”, alisema
Alisema ni wazi kila mmoja anatambua kuwa Serikali imekataa kutulipa fidia sisi wamiliki wa magari hivyo basi ni vema watambue kuwa mpaka sasa kampuni hiyo ya UDA ndio imehitaji kushirikiana nao.
Kitambi alisema katika makubaliano hayo mmiliki wa mabasi ambaye amejiunga na UDA hawataruhusiwa kujiunga na kampuni nyingine ya usafiri jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kuhusiana na njia ambazo hazijahusika na mradi wa mabasi yaendao kasi aliasema wana UWAMADA wataendelea kutoa huduma hadi hapo mpango mwingine utakapoanza.
Mjumbe huyo alisema pamoja na makubaliano hayo pia UWAMADA utakuwa na wajumbe wawili ambao watakuwa wakurugenzi katika bodi ya UDA.
Kitambi aliwataka wana UWAMADA waendelee kushikamana ili kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana na hakuna mtu ambaye ataonewa katika mchakato huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment