STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 30, 2014

Juventus yazidi kujichumbia kileleni Italia

Juventus celebrateAndrea PirloMABINGWA watetezi wa Serie A ya nchini Italia, Juventus, imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya usiku huu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Torino.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye mjini wa Turin, wenyeji walijikuta wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki waoStephan Lichtsteiner kulimwa kadi nyekundu kutokana na kupewa kadi ya pili ya njano.
Wenyeji hao walitangulia kuandika bao mapema kupitia kwa Arturo Vidal kwa mkwaju wa penati iliyotolewa na mwamuzi dakika ya 15 kabla ya wageni wao kurejesha bao hilo dakika saba baadae kupitia kwa Bruno Peres.
Wakati wengi wakidhani matokeo yangeisha kwa sare ya 1-1, kiungo mkongwe  Andrea Pirlo aliifungia Juventus bao muhimu la ushindi dakika za lala salama na kuifanya 'Kibibi' cha Turin, kufikisha jumla ya pointi 34 kutokana na michezo 13.
MUda mchache ujao wanaoshikilia nafasi ya pili AS Roma wenye pointi 28 watakuwa nyumbani kuwakaribisha Inter Milan katika pambano linalotarajiwa kuwa kali.

UWAJIBIKAJI! Polisi aliyeua kijana mweusi ajiuzulu!

Daren Wilson Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi nchini Marekani amejiuzulu. Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano. 
Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na kuuawa. Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28 aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.

Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo.''

Spurs yainyoa Everton mabao 2-1

Roberto Soldado
Roberto Soldado scores for SpursTIMU ya Tottenham Hotspur imetakata nyumbani baada ya kuinyoa Everton kwa mabao 2-1 katika pambano kali la Ligi Kuu ya England lililomalizika hivi punde.
Spurs iliyokuwa uwanja wa White Hartlane, ilishtushwa na wenyeji waliotangulia kuandika bao dakika ya 15 kupitia Kevin Mirallas kabla ya Christian Eriksen kusawazisha dakika ya 21 na Saldado aliongeza bao la pili dakika za nyongeza kabla ya mapumziko.
Kwa ushindi huo imeifanya Spurs kufikisha jumla ya pointi 20 sawa na wapinzani wao Arsenal isipokuwa wanakamata nafasi ya saba kwa tofauti na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena siku ya Jumanne kwa mechi sita ambapo Burnley itaikaribisha Newcastle United, Leicester itaialika Liverpool, huku Manchester United ikiikaribisha Stoke City na Swansea City ikiumna ana QPR, wakati Crystal Palace itaumana na Aston Villa na West Brom itapepetana na West Ham.
Jumatano kutapigwa mechi nne, Arsenal dhidi ya Southampton, Chelsea itailika Spurs, Everton itapepetana na Hull City na Sunderland itaialika watetezi Manchester City.

AC Milan yaifumua Udinese, Essien alimwa nyekundu

B3sxrK5IUAAcGQY Michael Essiens epic reaction to sending off during AC Milan v Udinese [video]
Michael Essien akiwa haamini kama kalimwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano
Italy Soccer Serie A
Jeremy Menez akifunga bao la Ac Milan
 MABAO mawili yaliyowekwa kimiani na Jeremy Menez, moja likiwa na mkwaju wa penati yametosha kuipa ushindi timu ya AC Milan katika pambano la Ligi Kuu ya Italia 'Serie A' dhidi ya Udinese.
Milan ikiwa nyumbani hata hivyo kama ilivyokuwa kwa wageni wao, walijikuta wakipoteza mchezaji mmoja baadaya Michael Essien kulimwa kadi mbili za njano, dakika chache tangu Udinese wampoteze Domizzi kwa rafu aliyomchezea Kaisuyke Honda na kusababisha penati ilifungwa na Menez katika dakika ya 65.
Menez aliongeza bao la pili dakikia 10 baadaye akimalizia kazi nzuri ya Boneventura na kuifanya AC Milan kukwea hadi nafasi ya tano ikiwa na pointi 21.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Cagliari ikiwa nyumbani ilijikuta ikifumuliwa mabao 4-0 na Fiorentina nayo Cesena pia ililala nyumbani kwa mabao 3-0 na genoa huku Empoli na Atalanta zilitoshana nguvu kwa kutofungana na Palermo ikitakata nyumbani kwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Parma na hivi sasa watetezi Juventus wapo nyumbani ikiumana na Torino na mpaka sasa ikiwa ni mapumziko matokeo ni 1-1.

Shabiki afa, Atletico Madrid ikiilaza Deportivo la Coruna

arda
SHABIKI mmoja wa soka amefariki dunia huko nchini Hispania kufuatia vurugu zilizotokea muda mfupi kabla ya mchezo kati ya Atletico Madrid na Deportivo La Coruna .
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alifariki dunia baada ya kupata shinikizo la damu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katikati ya vurugu zilizotokea kati ya mashabiki wa timu zote mbili.
Awali uongozi wa ligi ya Hispania ulijaribu kuahirisha mchezo huo lakini jaribio la kufanya hivyo lilizuiliwa na Shirikisho la soka la Hispania .
Picha ikiwaonyesha mashabiki wa Deportivo na Atletico madrid wakifanyiana vurugu saa chache kabla ya mchezo baina ya timu hizo mbili .
Picha ikiwaonyesha mashabiki wa Deportivo na Atletico madrid wakifanyiana vurugu saa chache kabla ya mchezo baina ya timu hizo mbili .
Vurugu kati ya mashabiki zilitokea saa tatu kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki kadhaa waliumia wakiwemo watu 10 ambao walipata majeraha yaliyohitaji kuwahishwa hospitalini .
Viongozi wa juu wa klabu zote 20 za ligi kuu ya Hispania wametoa tamko la kukemea vurugu zilizotokea baina ya mashabiki wa Deportive na Atletico Madrid nab ado haiajfahamika kama kuna hatua zozote zitakazochukuliwa kwa timu hizo kufuatia vurugu zilizotokea .
Mchezo huo uliendelea kama kawaida ambapo Atletico Madrid walishinda 2-0 baada ya mabao yaliyofungwa na Saul Nigez na Arda Turan.
Katika mechi nyingine Sevilla ikiwa nyumbani iliikwangua Granada kwa mabao 5-1 kwa sasa timu za
Cordoba na Villarreal zipo dimbani na baadae Valencia itaikaribisha Barcelona.

Kaka 'amchana' Emmanuel Adebayor kumtuhumu mama yake kumroga

ade n mum
Sakata linaloendela kati ya mshambuliaji star wa Totenham Emmanuel Adebayor  na mama yake mzazi anayefahamika kama Alice Adebayor limechukua sura nyingine baada ya ndugu wa mshambuliaji huyo kuingilia kati .
Ndugu huyo  anayeitwa Kola Adebayor ambaye ni kaka wa Emmanuel amesema kuwa madai ya mshambuliaji huyo ya kusema kuwa mama yao mzazi amemroga si ya  kweli.
Kola amesema kuwa kinachomfanya Adebayor kuamini kuwa mama yake amemfanyizia kwa waganga ili asiwe na bahati ni mawazo anayoyapata toka kwa watu wenye Imani ya dini ya kiislamu ambao wanamshauri vibaya nyota huyo .
Kola mwenye umri wa miaka 42 ambaye kazi ni dereva wa Malorry huko Ujerumani amesema kuwa amekerwa sana na kitendo cha mshambuliaji huyo kumuita mama yao mzazi mchawi kwani inaonyesha jinsi gani alivyokosa heshima kwa mzazi wake .
ade
Kwa mujibu wa Kola , Adebayor aliwafuata watu wanaojiita watakatishaji wa nafasi ambao kwa lugha ya kiingereza huitwa Spiritual Cleansers ili wamsaidie kwa sababu mambo yake hayaendi vizuri na kwa mshangao mkubwa watu hao walimwambia kuwa mama yake mzazi na dada yake ndio chanzo cha mikosi inayompata .
Kola anaendelea kusema kuwa Adebayor alifuata ushauri wa watu hawa na kuwafukuza dada na mama yake kwenye nyumba aliyojenga huko Afrika na tangu siku hiyo amegoma kuwatumia fedha za kujikimu .
Kwa upande mwingine dada wa Emmanuel Adebayor anayeitwa Maggie ndio aliyefichua sakata hili huko Ghana wakati akizungumza moja kwa moja kwenye kipindi cha radio ambapo alisema kuwa mchezaji huyo amemfukuza mama yake na ametelekeza tangu siku hiyo .
Kola Adebayor anadai kuwa mama yao mzazi tangu siku aliyofukuzwa hadi leo hii amekuwa akilia kila siku hali ambayo inahatarisha afya yake .
Mshambuliaji huyo amekanusha sakata hilo akisema kuwa sio kweli kuwa amemfukuza mama yake bali mama huyo ameamua kuondoka yeye mwenyewe , Adebayor ameongeza kuwa hayuko kwenye mawasiliano mazuri na mama yake kwani amekuwa akisambaza maneno kwa watu kuwa mambo hayatamwendea vizuri .

Man City yaipiga Southampton 3-0

Toure skips past the challenge of Southampton midfielder Victor Wanyama in the first half at St Mary's
Yaya Toure akichuana na mchezaji wa Southampton
Midfielder Lampard celebrates his fifth goal for the club with Aguero, after a typical finish from the edge of the box
Wachezaji wa City wakishangilia moja ya mabao yao lililofungwa na Lampard
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City jioni ya leo imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya 'wagumu' Southampton na kukwea hadi katika nafasi ya pili.
City, hata hivyo ilimaliza pambano hilo ikiwa pungufu kufuatia beki wake Eliaquim Mangala kulimwa kadi nyekundu baada ya kulimwa kadi mbili za njano.
Wageni walianza kuhesabu mabao yake katika dakika ya 51 baada ya kiungo Yaya Toure kuandika bao akimaliza kazi nzuri ya Sergio kun Aguero.
Bao la pili la City liliwekwa kimiania na mkongwe Frank Lampard dakiia ya 80 kabla ya dakika nane baadaye Gael Clichy kumaliza udhia kwa kuandika bao la tatu.
Ushindi huo umeifanya City kupanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 27, nane nyuma ya vinara Chelsea na wakiiporomosha Southampton waliokuwa wameng'ang'ania nafasi hiyo kwa muda mrefu ikiwa na pointi zake 26.
City itasafiri siku ya Jumanne kuifuata Sunderland ambayo jana iliikomaliza Chelsea na kutoka nao suluhu.
Ligi hiyo inaendelea tena muda huu kwa pambano jingine linalopigwa Uwanja wa White Hartlane kwa wenyeji Tottenham Hotspur wakiwa mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Everton.

Diamond aweka historia tuzo za Channel O

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIVUPj90sCe-xi1lGAmtEnUNWcQ20yj9jfRJVF30cfL1-o_qdrHJJEzLI-eDQqTYBZcfEDA6anCwlETFgQsVU0zLUJWC-PP5P8llZAXFy7SdINX7cQvnbDK6bttBVHRGCI6hb4dmHZNys/?imgmax=800
MSANII nyota wa muziki wa kizzi kipya nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' juzi Jumamosi aliweka historia baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo tatu za 'Channel O Music Video Awards' (CHOMVA-2014).
Diamond mshindi wa kihistoria wa tuzo za Kili Music Awards 2014 baada ya kunyaku tuzo saba kwa mpigo aliweka rekodi hiyo kwenye ukumbi wa  Nasrec Expo Centre, nchini Afrika Kusini zilipotolewa tuzo hizo.
Staa huyo wa 'Nitampata Wapi', 'Mdogomdogo' na 'My Number One', alishinda tuzo tatu kati ya nne alizokuwa akiziwinda katika vipengele vya  Most Gifted East, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer.
Hii tuzo ya tatu ya kimataifa kwa Diamond kwa mwaka huu baada ya awali kunyakua tuzo ya AFRIMMA na Kora Music (ambayo hata hivyo mpaka sasa imekuwa na na utata).
Orodha kamili ya washindi wa tuzo hizo za Channel O ni kama ifuatavyo;
Most Gifted R&B video ni Crazy but Amazing-Donald, Most Gifted West Video
ni ‘Turn Up-Olamidem, Most Gifted Ragga/Dancehall ni Buffalo Soulja na The Most Gifted Kwaito akiwa ni  Uhuru ft Oskido & Professor Kalawa -tjukutja.
Tuzo nyingi kama za Most Gifted East Video ni Diamond Platnumz, Most Gifted Dance Video ni Busiswa-Ngoku, Most Gifted Hip Hop Video ni AKA- Congratulate, Most Gifted Newcomer akiwa ni Diamond Platnumz tena.
Katika kipengele cha Most Gifted Male Video mshindi ni Casper Nyovest-Doc Shebeleza, Most Gifted Female Video alikuwa Tiwa Savage-Eminado, Most Gifted Afro Pop Video ni Mtanzania Diamond Platnumz, Most Gifted duo/group/featurning ni KCEE ft Wizkid-Pull Over na Most Gifted Video of the Year alikuwa ni Carsper  Nyovest- Dos Shebeleza.

Saturday, November 29, 2014

Arsenal yainyoa kiduchu West Brom Albion nyumbani kwao

The England international rose highest to head the Gunners in front after Ben Foster failed to keep out his attempt
Danny WElbeck akiifungia Arsenal bao pekee
Arsenal players celebrate after finally breaking down West Brom with Danny Welbeck's header on the hour mark at the HawthornsBAO pekee la lililofungwa na mshambuliaji Danny Welbeck limeisaidia Arsenal kupata ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya West Bromwich Albion.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa The Hawthorns, WElbeck alifunga bao hilo kwa kichwa katika dakika ya 59 akimalizia kazi nzuri ya Santi Cazorla na kuipa ushindi huo muhimu Ze Gunnerz.
Ushindi huo umewafanya vijana wa Arsene Wenger kuchumpa hadi nafasi ya nne, ingawa mechi nyingine zinachezwa jioni hii.
Wenyeji walikaribia kusawazisha bao hilo dakika ya 80 baada ya kugongesha mwamba mkwaju wake murua ambao ulionekana kuelekea wavuni.
Kipigo hicho kimeifanya West Brom kufikisha mechi saba ikicheza nyumbani bila kupata ushindi na katika mechi ya leo mashabiki wao walishindwa kuwavumilia na kuanza kuwazomea.

Angel di Maria, Yaya Toure kuchuana World X1 2014

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/10/25/1414241023993_wps_6_Manchester_United_s_Angel.jpg
di Maria
http://www.kora.me/uploads/jpg/toot_dfc8f07f1c.jpg 
WACHEZAJI 15 wa nafasi ya kiungo wametangazwa na Shirikisho la Soka Duniani,FIFA  kwa ajili ya kupigiwa za kuchaguliwa kwenye kikosi cha dunia ambapo majina matatu pekee ndio yatashinda nafasi hiyo. 
Kikosi hicho kinachojulikana kama World XI 2014, ambacho huteuliwa kwa kura za wachezaji duniani kote kinatarajiwa kutangazwa rasmi katika sherehe za utoaji tuzo ya Ballon d’Or Januari 12 mwakani. 
Wote waliojumuishwa katika orodha hiyo ni nyota waliokuwemo katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil akiwemo mfungaji bora James Rodriquez wa Colombia pamoja na Angel Di Maria ambaye timu yake ya Argentina ilishika nafasi ya pili pamoja na Bastian Schweinsteiger anaewawakilisha mabingwa wa dunia Ujerumani. 
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wao wanatarajiwa kuwemo katika orodha ya washambuliaji ambayo itatolewa Desemba mosi mwaka huu, wakati wateule wa nafasi ya golikipa na mabeki wao wakiwa tayari wameshatangazwa. 
Orodha kamili ya viungo hao na timu zao ni pamoja na Xabi Alonso (Bayern Munich), Angel Di Maria (Manchester United), Cesc Fabregas (Chelsea), Eden Hazard (Chelsea), Xavi (Barcelona) na Andres Iniesta (Barcelona).
Wengine ni; Toni Kroos (Real Madrid), Luka Modric (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (IJuventus), Paul Pogba (Juventus), James Rodriguez (Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Yaya Toure (Manchester City), Arturo Vidal (Juventus)

Mke wa Idd Kipingu amwaga misaada shule za Montesory, Ulongoni

Mkurugenzi wa Zugo Gold Mining na Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho na Ngumi za Ridhaa Tanzania (*BFT), Zuwena Idd Kipingu akizungumza na wazazi kwenye hafla ya Mahafali ya 35 Shule ya Montesoty Nursery& Primary iliyofanyika leo
Mkurugenzi wa Zugo Gold Mining na Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho na Ngumi za Ridhaa Tanzania (*BFT), Zuwena Idd Kipingu akizungumza na wazazi kwenye hafla ya Mahafali ya 35 Shule ya Montesoty Nursery& Primary iliyofanyika leo

Baadhi ya wazazi waliohudhuria Mahafali ya 35 ya Shule ya Montesory wakifuatilia maonyesho ya watoto wao
Baadhi ya wazazi waliohudhuria Mahafali ya 35 ya Shule ya Montesory wakifuatilia maonyesho ya watoto wao
Baadhi ya wahitimu wa shule ya Montesory wakionyesha maonyesho ya kitaaluma
Wahitimu wa Montesory wakiimba kwenye sherehe za kuagwa zilizofanyika shuleni hapo mchana wa leo

Wanafunzi wakionyesha michezo yao ya taaluma. Hapa wanaigiza kama wapo darasani na mwalimu wao aliyekaa pembeni kushoto


Ikafuata burudani na kurudi 'magoma' hawa majamaa ni noma
Sabri Omary akionyesha umahiri wa kunengua katima mahafali hayo

Babu na wajukuu zake wakisimuliana hadithi kwa vitendo, Kuku na Bata wakimsikiliza Tembo
Kama Muuguzi vile, mmoja wanafunzi wahitimu wa Montesory akijitambulisha kuwa ni Muuguzi kwa sababu ya kupata elimu...hilo ni onyesho la taaluma







Watoto wakikabidhiwa vyeti na zawadi zao

SHULE za Montesory na Ulongoni B zilizopo wilaya ya Ilala zimepewa kwa nyakati tofauti misaada ya tani moja ya Saruji sambamba na fedha taslim kwa ajili ya kuboresha majengo ya shule hizo.
Misaada hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Zugo Gold Mining ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake na Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Idd Kipingu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule hizo mwishoni mwa wiki.
Akizungumza kwenye mahafali ya 35 ya wanafunzi wa awali wa Shule ya Montesory, Zuwena alisema kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapoa wasaa wa kusoma katika mazingira mazuri anajitolea tani moja ya simenti na Sh,. Mil. 1 kwa ajili ya kuendelez aujenzi wa shule hiyo iliyopo Ilala Boma.
Zuwena aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Anna Mkapa katika mahafali hayo kama mgeni rasmi na kutangaza kutoa msaada huo ikiwa ni siku moja tu tangu akabidhi msaada kama huo katika Shule ya Ulongoni B.
"Bila kusubiri kuombwa nimeona majengo yenu hayajamalizika, hivyo najitolea kuwapa tani moja ya saruji na Jumatatu tuwasiliane ili niwakabidhi pamoja na Sh Milioni 2 za vifaa vya michezo na Sh Mil 1 ya kusaidia ujenzi huo," alisema.
Aliongeza kuwa, kama mmoja wa wanawake waliofanikiwa kujiendeleza kimaisha kupitia michezo anawasihi wazazi nchini kutowakataza watoto wao wenye vipaji mbalimbali kujihusisha na vitu vinavyohusiana na vipaji vya ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujiajiri kupitia fani hizo.
Alisema yeye wakati akiwa mtoto alikuwa akichapwa mno na baba yake kwa kupenda kwake michezo, lakini alikuja kuwa mwanamke wa kwanza kunyakua mkanda mweusi katika karate na taekwondo na kuwa mfanyabishara mkubwa kwa sasa kutokana na fursa aliyopata kupitia kwenye michezo.
"Wazazi wasikazanie watoto wao kusoma tu, pia wawasaidie kuendeleza vipaji vyao kwa nia ya kuwatengenezea ajira wanapokuwa wakubwa," alisema Zuwena.
Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 75 walihitimu masomo yao ya awali na kukabidhiwa vyeti pamoja na zawadi na mgeni rasmi huyo Zuwena Idd Kipingu, sambamba na kutoa burudani mbalimbali za taaluma na michezo.

Thursday, November 27, 2014

Waziri wa Nishati ajitetea bungeni kuhusu jinamizi la Tegeta Escrow


profmuhongoWAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewasilisha utetezi kwenye Bunge la Jamhuri kuhusiana na kutajwa kwake kuhusika na sakata ya wizi wa mabilioni ya fedha la Tegete Escrow.
Awali Waziri huyo alianza kwa kuomba radhi kama jana kulikuwa na usumbufu wa umeme na anawaagiza mameneja wote wa TANESCO wasikate umeme.
Anatoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow, mengi yamesemwa na ni wakati wa kuanza mjadala kujua ukweli, Shukrani kwa CAG, TAKUKURU kwa uchunguzi. Pia nawashukuru PAC, jana tulitulia kuwasikiliza PAC na leo tutulie tusikilize utetezi wangu.
Miaka ya 1990 tulikuwa tuna upungufu wa umeme kutokana na maji, 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa inamilikiwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na 30% na Mechmar ya Malaysia 70%.

Kulingana na mkataba, majukumu ya IPTL yalikuwa kujenga, kumiliki na kuendesha hivyo utaifishaji utaiingiza serikali katika matatizo makubwa ikiwemo kushtakiwa kimataifa pia itafukuza wawekezaji binafsi. TANESCO na IPTL walisainiana mkataba wa miaka 20, hata hivyo uzalishaji haukuanza mara moja kutokana na mgogoro ulioibuka baina ya TANESCO na IPTL
IPTL ilianza kuzalisha umeme 2002 hivyo mkataba ukaanza kuhesabiwa hapo, kutokana na mgogoro ikafunguliwa Escrow Account na Escrow ilizungumziwa toka mkataba wa 1995.Kusoma zaidi bofya

2004 TANESCO ilifungua shauri kupinga tozo la capacity charge

Taarifa hii sio ya kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua kesi yoyote dhidi ya Standard Charted kama ilivyosemwa na PAC. Kesi hiyo ilifunguliwa na Standard Charted na ilikuwa haihusu capacity charge. Hamna kokote mkataba kati ya Standard Charted na TANESCO.
Makinda ameingilia na kusema ripoti itatolewa baada ya wabunge kudai ripoti hiyo.
Muhongo anaendelea
Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30, na uamuzi haujabadilishwa na mahakama yoyote. 2004 kampuni ya Mkono and CO Advocates iliishauri TANESCO iendelee kupinga capacity charge London. Hata hivyo, haikuishauri TANESCO kufungua kesi za TANZANIA wala mahakama ya kimataifa. Hadi 2013 Jaji Utamwa anatoa hukumu ya mgogoro wa wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu tozo ya IPTL.
UUZAJI WA HISA ZA VIP
Kutokana na kutokubaliana Mechmar iliishauri VIP ifungue shauri. VIP ilifungua shauri Tanzania ikiomba IPTL ifilisiwe. Uamuzi ulitolewa kwa shauri la VIP. Chini ya Kimario, alpewa mfilisi wa muda kulinda mali za IPTL, kufanya uchunguzi ili mahakama iweze kutoa uamuzi. Uamuzi ulitoka IPTL iweke kwenye ufilisi kamili chini ya RITA. Hukumu ilipingwa mahakama ya rufaa ikianisha dosari katika uamuzi wa mahakama kuu na Standard Charted Hong Kong. Mahakama ya rufaa ilikubaliana na hoja hiyo na ilipelekwa tena kwa mfilisi wa muda kukusanya madeni, kusuluhisha mogogoro na kuendesha mitambo ya IPTL kwa niaba ya IPTL.

Serikali haiwajibiki kuingilia hisa za makampuni binafsi, mauzo ya hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu endapo yatatambuliwa na BRELA. Uhamishaji wa hisa 7 ulisajiliwa hapa nchini. Kamati katika uthibitisho huo inakubali hisa za Mechmarr unamilikiwa na PAP.
Hisa saba za IPTL zinatambuliwa pia na Standard Charted, Kama PAP haimiliki asilimia sabini kwa nini wana makubaliano na Standard Charted ya Uingereza?
Ilifilisiwa Malaysia na sio Tanzania, madai ya Standard Charted dhidi ya TANESCO ni kwa sababu IPTL waliweka dhamana mtambo wa kuzalishia umeme, Lakini benki ya Hong Kong ilikosa sifa ya kufungua shauri Tanzania hivyo ilifungulia Uingereza.
VIP chini ya usuluhishi wa RITA iliuza hisa zake PAP kwa dola milioni 70 na ndivyo ilivyomaliza mgogoro wa IPTL. Mimi sio dalali wa hii biashara bali ni dalali wa (anasema mambo mazuri aliyoyafanya)
Makinda amekuwa mkali kidogo kwa Muhongo asome taarifa na asiseme ambayo hayamo.

AKAUNTI YA ESCROW
TANESCO kwa ushauri wa Mkono walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme na makadirio ya mtaji walitoa notisi (Invoice disputes notice) ya kupinga usahihi wa malipo. Alietoa ushauri ni kampuni ya Mkono, 2006 serikali ulisaini mkataba wa kufungua Akaunti ya Escrow.

MMILIKI WA FEDHA YA ESCROW
Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO. PAC walitoa mapendekezo kuwa imethibitisha kuwa mchakato wa kutoa pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kutakatishwa na benki mbili

TAHADHARI ZILIZOCHUKULIWA
Serikali ilichukua kinga kutoka IPTL, kwa mujibu wa kinga IPTL itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na mwanasheria mkuu wa serikali. (Yoyote anaedai chochote aende IPTL)

PAC wameeleza serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha juu ya madai mapya kama yangejitokeza kitu ambacho sio kweli.
DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba IPTL inaidai 321 Bilioni, bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya.

Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.
Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake unategemea maamuzi.
MADENI TANESCO
Wazri Muhongo amesema Tanesco haijaanza kutengeneza pesa kwa manufaa ya Umma ina madeni. Hivyo hamna fedha za umma popote kuna madeni tu.

MWANASHERIA WA TANESCO

Prof. Muhongo amesema Mwanasheria wa Tanesco anayedaiwa kufukuzwa kazi taarifa hiyo si ya kweli na bwana huyo amedanganya umma.
Ukweli ni kwamba Mwanasheria huyo alileta ombi la kusafiri kwenda Malaysia kwa kumdanganya mwajiri wake kwa kuandika barua kuwa anakwenda na Mwanasheria Mwandamizi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Hivyo hakufukuzwa kazi bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kumwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mwezi Februari mwaka huu#TegetaEscrow
BUNGE LAAHIRISHWA

Spika wa Bunge, Anne Makinda ameahirisha kikao cha bunge mpaka jioni saa 11 baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo kumaliza kutoa utetezi wa serikali.
Chanzo:Mwananchi.

Newz Alert! Watu 11 wapoteza maisha katika ajali mjini Tanga


Taswira kutoka eneo la Mkanyageni baada ya ajali hiyo mbaya iliyoua watu 11.

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa watu 11 wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali mbaya eneo la Mkanyageni mkoani Tanga.
Inadaiwa kuwa ajali hiyo ilisababishwa na gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana na Scania namba T 605 ABJ asubuhi hii.
Katika ajali hiyo, Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kwenda Lushoto na madereva wa magari yote mawili hawajulikani walipo baada ya ajali.
Miili ya marehemu katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, Tanga.

Taarifa zaidi zitawajia baadaye ila MICHARAZO inatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hiyo na kuwaombea waliitangulia mbele ya Haki Roho zao ziweke mahali Pema na majeruhi wapone haraka.

Arsenal yasonga mbele, Liverpool yabanwa Ulaya, Real yaua

The Arsenal players celebrates the French youngster's early goal in the Champions League Group D clash

Alexis Sanchez runs towards the Arsenal fans in celebration of his second-half strike against Borussia DortmundGerrard wins a tussle for the ball with Marcelinho (left) of  Ludogerets at the Vasil Levski StadiumLambert celebrates with Joe Allen as his goal made it 1-1 at the at Vassil Levski StadiumIt wasn't just fans Ronaldo had to watch out for as he is tackled hard by Basle's Fabian Schar during the gameBale gets in front of his man from a corner but is unable to find the back of the net for RealRonaldo wheels away after bundling home from close range to give Real the 1-0 lead at St Jakob ParkWAKATI Arsenal wakitinga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi nyumbani, Liverpool imejikuta ikibanwa ugenini kwa kuambulia sare.
Arsenal walipata ushindi muhimu nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund kwa kuwalaza mabao 2-0 wakati Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets .
Mabao ya Yaya Sanogo na jingine la Alexis Sanchez yalitosha kuivusha Arsenal hatua hiyo katika mechi kali iliyochezwa uwanja wa Emirates.
Arsenal imeungana na Wajerumani hao kutinga hatua ya 16 Bora kutoka kundi D baada ya kufikisha pointi 10, tatu nyuma ya Dortmund inayoongoza kileleni.
Nao Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogoretsna kuzidi kujiweka pabaya katika azma yao ya kucheza hatua ya mtoano.
Ludogorets waliwashtukiza wageni wao kwa kupata bao la mapema la dakika tatu kupitia Dani Abalo kabla ya Liverpool kusawazisha dakika tano baadaye kupitia Rickie Lambert na baadaye Jordan Henderson kuwapa uongozi wa 2-1 wageni.
Hata hivyo Vijogoo vya England walishindwa kulinda bao lao baada ya kuruhusu wenyeji kusawazisha dakika mbili kabla ya mchezo huo kumalizika baada ya Georgi Teziev kuifuingia Lodogorets.
Sare hiyo imeifanya Liverpool kufikisha pointi nne na kushika nafasi ya tatu ikitanguliwa na Basel iliyolazwa  bao 1-0 na Real Madrid iliyotangulia 16 Bora ikiongoza kundi B.
Bao la Real lilifungwa na Ronaldo na kumfanya Mreno huyo kumfikia Raul katika orodha ya waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo wakishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi anayeongoza kwa mabao 74 dhidi ya 71 na wakali hao.
Katika mechi nyingine Zenit iliitambia Benfica kwa kuilaza bao 1-0, huku Atlético Madrid ikiendeleza rekodi yao ya kutofungwa uwanja wa nyumbani kwa kuicharaza Olympiakos Pirates kwa mabao 4-0 na kufuzu 16 Bora.
Wakali wa Italia, Juventus wakipata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Malmo, huku Monaco ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya   Bayer Leverkusen, huku Anderlecht ikiinyoa Galatasaray kwa mabao 2-0.
Mpaka sasa wakati michuano hiyo ikisaliwa na raundi moja kabla ya kufikia tamati hatua ya makundi timu nane ndizo zimejihakikisha hatua inayofuata zitakazochezwa mwezi ujao.
Timu hizo ni pamoja na Atletico Madrid, Real Madrid na  Barcelona zote za Hispania, Chelsea na Arsenal za England, Bayern Munich na Borussia Dortmund za Ujerumani, PSG ya Ufaransa, POrto ya Ureno na Shakhtar Donetsk ya Uturuki.

Real Madrid, Bayern waongoza tuzo za Kikosi Bora Ulaya

http://english.ahram.org.eg/Media/News/2014/4/24/2014-635339446265357238-535.jpgKLABU ya Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wamethibitisha ubora na thamani yao baada ya kutoa wachezaji nane katika uwaniaji wa tuzo ya kikosi bora cha Ulaya.
Tuzo hiyo ya Uefa ya mwaka 2014 itakayotolewa hivi karibuni inajumuisha pia wachezaji wanne kutoka AtleticoMadrid ambao pia wanaiwania.
Wanaowania kuingia kwenye 1st Eleven ya mwaka ya Uefa ni kama ifuatavyo;
Kutoka Madrid : Carvajal, Ramos, Kroos, Modric, James, Bale, Benzema na Cristiano Ronaldo.
Bayern wenyewe wametoa wachezaji sawa kama Real Madrid nao ni Neuer, Alaba, Benatia, Boateng, Lahm, Xabi Alonso, Müller na Lewandowski.
Upande wa Atletico Madrid iliyotoa wachezaji wanne ambao ni Koke, Arda, Godín na Miranda.
Wengine waliopo kwenye kinyang'anyiro hicho ni Xabi Alonso (Bayern Munich) na Di María (Manchester United), Courtois (Chelsea), Diego Costa (Chelsea).
Kwa upande wa Barcelona imetoa wachezaji watatu ambao ni Rakitic, Neymar na Messi. Pia mchezaji wa Red Bull Salzburg Jonathan Soriano naye yupo kwenye mbio hizo za kuwepo kwenye First Eleven.