STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

ES SETIF MABINGWA WAPYA AFRIKA, AS VITA YAKWAMA

KLABU ya ES Setif ya Algeria imeweka historia ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1988 baada ya kuishinda AS Vita ya DR Congo kwa uwiano wa bao la ugenini.
Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufunga bao 1-1 katika mechi ya marudiano mwishoni mwa wiki na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-3 baada ya awali timu hizo kutoka sare ya 2-2 mjini Kinshasa.
Katika mechi iliyochezwa uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida, wenyeji walianza kutangulia kupata bao dakika ya nne tu ya kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes aliyemaliza pasi ya El Hadi Belameiri.
AS Vita iliyokuwa ikiliwinda taji hilo kwa udi na uvumba baada ya kufanikiwa kutinga fainali baada ya miaka mingi kupita, ilirejesha bao hilo dakika tano baadaye kupitia kwa Lema Mabidi kwa mkwaju mkali nje ya penati.
Mabidi ndiye aliyefunga mabao mawili wakati Vita ikilazimishwa sare nyumbani wiki iliyopita.
Kufungwa kwa bao hilo kuwafanya wenyeji kuanza kujiangusha kwa nia ya kupoteza muda na hatimaye kufanikiwa kumaliza dakika 90 wakiwa mabingwa wapya baada ya miaka 26 iliyopita.

No comments:

Post a Comment