STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

Sitta 'amng'ong'a' Jaji Warioba vurugu za jana

Samuel Sitta, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6YLIzt5yxM8bGdMOOt4NZ7sOY_QCkcA60TVGri9nIvQHC_VMnTvoDja22z1RugAn-oF2QnW7FV5SRtaVkjFrSKYDcipeS2QhhWNrpQXfNU6L0K5mSZn6K7BAxRgIvq3nhXT-tBHp1pzc/s1600/05WARIOBAAFANYIWAFUJO5.jpg
Jaji Warioba jana kabla ya kufanyiwa vurugu na watu wanaodaiwa kupangwa na watu wasiofurahishwa na msimamo wake wa kutetea wananchi baada ya kuchakachuliwa kwa maoni yao kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiongoza.
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa na Redio Voice of Tabora, inayomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Tabora, Ismail Aden Rage kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.


Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.
Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.
Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
(MALUNDE)
Kuvamiwa kwa Jaji Warioba kuleta hisia kwamba ni 'chuki' dhidi yake katika kueneza ukweli juu ya kilichofanywa na wajumbe wa Bunge la Katiba Maalum katika Katiba Pendekezwa ambayo imeachja baadhi ya maoni ya wananchi na kuwekwa mawazo ya wajumbe hao ambao wengi wao ni wa chama tawala (CCM).
Kadhalika watu wamekuwa wakihoji inakuwaje Waziri Mkuu Mstaafu anaweza kufanyiwa uhuni kama ule uliofanyika Blue Pearl kama HAKUNA NGUVU nyuma ya vijana WALIOHUSIKA?!
MICHARAZO ina HAMU kubwa ya kuisikia SERIKALI itatoa TAMKO gani juu ya UHUNI aliofanyiwa WAZIRI MKUU MSTAAFU, Jaji Joseph Warioba kwani siyo kitu cha kawaida kwa wananchi waliostaarabika na wenye kudumisha udugu, umoja na mshikamano hata kama watu WANATOFAUTIANA mawazo. Ngoja tuone.
Makonda mwenyewe amekanusha taarifa za kuhusika na vurugu hizo za jana akidai hajampinga Jaji Warioba kama mitandao mingine ya kijamii ilivyoripoti na pia amejitetea alikuwa akimsaidia Jaji mstaafu huyo ili asipate madhara na kwamba anamuheshimu kama BABA YAKE MZAZI.

No comments:

Post a Comment