MVUA kubwa iliyonyesha jijini Tanga imekwmaisha pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Mgambo JKT na Mbeya City kushindwa kufanyika kwenye uwanjka wa Mkwakwani na badala yake kipute hichio kitachezwa leo.
Mchezo
huo uliokuwa uchezeshwe na refa Israel Mujuni Nkongo uliamriwa kuharishwa hadi leo kutokana na hali ya uwanja kutoruhusu ambapo hata mashabiki walikosa mahali pa kujikinga dhidi ya mvua kubwa iliyonyesha mapema asubuhi na kukata kabla ya kurudi tena jioni kwa nguvu kubwa.
Kwa
mujibu wa msimamizi wa mchezo huo mwamuzi mstaafu Hamisi Kisiwa mara
baada ya ukaguzi kufanywa na waamuzi wa mchezo huo iliamuriwa mchezo huo
kusogezwa mbele kwa saa 24 kwa mujibu wa kanuni huku taarifa zaidi
ikisubiriwa kutoka kwa wasimamizi wa ligi hiyo bodi ya ligi.
Mbeya City inakutana na Mgambo ikiwa imetoka kujeruhiwa nyumbani katika katika mechi dhidi ya Azam, wakati Mgambo bado wanachekelea ushindi wa bao 1-0 iliyopata mjini Mtwara mbele ya Ndanda Fc
No comments:
Post a Comment