STRIKA
USILIKOSE
Sunday, December 14, 2014
Azam yaanza vibaya Uganda, yanyakua kifaa kipya
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, Azam imeanza vibaya ziara yao nchini Uganda baada ya kufumuliwa mabao 3-2 na SC Villa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Azam, Jemedari Said akihojiwa na kituo kimoja cha redio kutoka Kampala, alisema kuwa katika mechi hiyo Azam walienda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.
Jemedari alisema walianza kufunga wao bao dakika za mapema kupitia Mrundi Didier kavumbagu kabla ya wenyeji kusawazisha na kipindi cha pili waliporejea Azam waliongeza bao la pili dakika hya 65.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Khamis Mcha 'Vialli' kabla ya wenyeji kutumia dakika 10 za mwisho za pambano hilo kurejesha bao la pili na kuongeza bao la ushindi katika dakika za 81 na 83.
Meneja huyo alisema kuwa Azam itashuka tena dimbani siku ya Jumatano kwa kuumana na URA, pambano likichezwa kwenye uwanja wa KCC, mjini Kampala.
Katika hatua nyingine klabu hiyo imemsajili winga machachari wa KCCA, Brian Majwega mkataba wa miaka miwili baada ya kocha Joseph Omog kuvutiwa naye.
Majwega anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Azam FC katika dirisha dogo baada ya beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, ambaye amesainiwa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment