Kanisani alipouawa mwalimu Ng"wandu |
KWA kipindi cha miezi miwili tu, kuanzia Octoba 9 hadi Desemba 4 mwaka huu, ambapo jumla ya vijana 6 wameuawa katika mazingira ya kutatanisha, watatu
wamechinjwa katika kata ya Kitendaguro, 1 katika kata ya Rwamishenye,
huku wawili wakichinjwa katika kata ya Kibeta ndani ya manispaa, huku
wananchi wakishangaa ukimya wa mamlaka bila kuchukua hatua.
Tarehe
09 Oktoba, aliyeuawa mwalimu DIONIZ NGW’ANDU wa shule ya sekondari
Kagemu, alipokuwa katika kanisa la PAGT, baada ya kukatwa kichwa na kitu
chenye ncha kali, huku jamaa yake aliyekuwa mlinzi katika kanisa hilo
siku hiyo akijulikana kwa jina mojala THEMISTOCRES akisalia na ulemavu
wa maisha, kama alivyoeleza mchungaji wa kanisa hilo FAUSTINE JOSEPH.
Siku
kati ya 5 au saba badaye, mwili wa kijana ambaye hakutambuliwa majina
wala sura, ulikutwa umeharibiwa kwa kunyofolewa macho, huku ukitupwa
kando mwa shamba la mmoja wa wakazi wa Kitendaguro, ambapo Anakret
Laurent Kyaishozi miaka 30 alikuwa shuuda, aliueleza mtandao huu kuwa
mwilihuoulichukuliwa na polisi mpaka sasa hawajajua ninikiliendelea.
Kando
na hayo, familia ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 37 Erick Kashaga
akiacha mjane Sofia Mozes miaka 32 na watoto saba, imesalia katika
mvutano mkubwa,na familia ya bwana Levocatus , ambaye mpaka sasa yuko
mikononi mwa jeshi la polisi, huku jamaa zake wakielezwa kuwa uchunguzi
unaendelea.
Kaburi la Mozes Kashaga |
Levocatusi ni kijana mwenye
umri wa miaka 33 huku akiwa na watoto watatu wawili wakizaliwa na mke
wake wa Katoma walieachana, na mmoja akizaliwa na mke anayeishi naye
Kitendaguro, Bi Ajat au Betrida mwenye umri wa miaka 32, alikamatwa
baada ya kutajwa kuwa alitambuliwa na kijana aliyekuwa na marehemu
wakatiwa tukio .
Mzee Rumumba akionesha eneo alipochinjwa Mozes |
Mzee
SILIDION RUMUMBA mwenye umri wa miaka 73, ndiye mmiliki wa kilabu cha
pombe, ambacho dakika za mwisho marehemu aliondoka hapo muda wa saa tano
usiku, akiwa na jamaa zake wawili.
Ndani
ya dk kama mbili baadaye, liyetajwa kwa jina moja tu la Eriki alirudi
nyumbani kwa mzee SILIDION RUMUMBA akiwaeleza kuwa wamevamiwa na mtu
ambaye alimtaja jina, huku akisema kuwa hana hakika kama watamkuta hai
Kashaga, ilhali akitoa taarifa hizo kimyakimya, pasi na kupiga kelele
wakati wa tukio,jambo ambalo linawashangaza wengi, kwasababu marehemu
ameuawa karibu kabisa na makaazi ya watu.
Mama mzazi wa Mozes |
Kando
na maelezo hayo, nimetaka kusikiliza ushuuda wa Erick aliyethibitisha
kuwa alishuudia mauaji hayo, lakini nyumbani kwaojamaa zakewalisema kuwa
huwezi kumwona sababau wamemficha sehemu baada ya kutishiwa na mkewa
mtuhumiwa.
Hayo
yamesalia katika familia hizo ndani ya kata ya Kitendaguro, huku katika
kata ya kibeta, lawama kubwa zikiangushwa kwa mamlaka, kuwa
hawajaonesha juhudi zozote baada ya kuuawa kijana GOODRUCK FRANCIS
aliyekuwa na umri wa miaka 38, ambapo taarifa za awali zinaonesha kuwa
aliuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana, ikiwa ni kando kando
mwa barabara ya mtaa wa Kibeta Amjuju.
Bi
Stella Lenatus amesema amekata tama kwasababu tangu ahojiwe, ameenda
kituoni kujua taarifa za mdodgo wake na kuambiwa asubiri walikuwa bize
na kazi nyingine muhimu.
Hapo kustoto pichani ndipo aliuawa Gudrack eneo la Kibeta Anyama. |
Sambamba
na wanaouawa pasipo kutambulika majina na makwao ndani ya manispaa ya
Bukoba, Ernest Kato ni kijana aliyeuawa mwezi novemba akiwa na
miaka32,katika mtaa wa Bugezi kata Rwamishenye, majira ya usiku, na
kutambulika asubuhi ya tarehe iliofuata kwa kukutwa amechinjwa, huku
akiacha mjane na mtoto mmoja, ambaye hatahivyo amekimbia kwa kuhofia
naye kuawa.
Mmoja
kati ya wanafamilia wa marehemu Ernest, ameomba jina lake lihifadhiwe,
pamoja na kusema kuwa wanaishi kwa hofu kubwa kiasi cha kujipangia muda
wa kurudi nyumbani mapema nyakati za usiku, na shughuli zimesimama.
Mauaji
ya mwisho hadi ninakamilisha makala haya, ni alivyouawa Joran
Rutulaniisa, mkaazi wa Kibeta magoti, nilifika eneo la tukio muda mfupi
tu baada ya polisi kuubeba mwili wake lakini taarifa za ndugu ambao
hatahivyo wanahofu ya maisha yao, ni kuwa nduguyao ameuawa kwa aina ile
ile ya vifo vya kukatwa koromeo.
Marehemu Rutu enzi za uhai wake |
Tetesi
ambazo bado sijazithibisha, wananchi wanaofanya biashara ya senene,
wamelazimika kuanza kujifunga vitu vigumu na tauro shingoni, kama
taadhali watakapovamiwa.
Shangazi na mama mdogo wa marehemu kwenye kaburi la Rutu |
Baba wa marehemu Rutulanisa |
Mauaji
nikitendo kisichokubalika kwa mwenyezi Mungu, jambo linalompa shekh
mkuu wa mkoa wa Kagera Aruna Kichwabuta,kukemea hali hiyo katika mamlaka
na wananchi.
Shekh mkuu wa mkoa, Haruna KICHWABUTA |
Makala maalumu sehemu ya kwanza kuhusu mauaji hayo inaruka marudio leo saa moja jioni kupitia 88.5 Kasibante fm Bukoba.
Na Mwanaharakati
No comments:
Post a Comment