SHIRIKISHO la Soka Duniani, FIFA, linatarajia kupiga kura ili kuamua kuweka hadharani ripoti ya Uchunguzi wa Mgogoro wa Rushwa katika utoaji wa zabuni ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 na 2011.
Zoezi hilo la upigaji wa kura unatrajiwa kufanywa wiki ijayo, ili kumaliza mzizi wa fitina ambayo umelighubika shirikisho hilo kwa siku za karibuni.
Mkutano huu utakaofanyika jijini Marrakesh, Morocco
utatoa maamuzi ya kuweza kusambazwa ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya
rushwa katika kutoa nafasi ya wenyeji wa michuano ya kombe la dunia.
Viongozi wa soka chini ya mapendekezo ya kamati ya maadili ya FIFA
ilisisitiza siyo rahisi kutolewa kwa ripoti hiyo kwa sababu za kisheria.
FIFA wamewapa nafasi Urusi kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na
Qatar kwa mwaka 2022, uteuzi wa nchi hizi unaonekana umegubikwa na
mazingira ya rushwa na kusababisha kumweka katika wakati mgumu Rais Sepp Blatter anayetarajiwa kuwania tena nafasi hiyo.
Hivi karibuni Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya, UEFA, Michel Platini alimtaka Rais huyo wa FIFA, kupisha wengine na kuweka bayana hatampigia kura labda kama atajitokeza mgombea mwingine wa tatu.
No comments:
Post a Comment