Mwadui Shinyanga |
Aficans Sports 'Wana Kimanumanu |
KLABU za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatarajiwa
kucheza mchezo wa fainali kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
African
Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa
kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya
Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Baraka Kizuguto alisema kwa mujibu wa Kanuni, ni lazima apatikane mshindi mmoja
ambaye ni bingwa.
“Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi
Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC,
Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans,”alisema.
Alisema
timu za Green Worriors na Villa Squad
zimeteremka Daraja la pili baada ya
kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad
kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.
Katika
hatua nyingine, Rais wa TFF Jamal Malinzi
ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) ,
Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu
zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Katika
salamu zake Malinzi alisema klabu hizo zinapaswa
kujipanga na kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom
2015/2016, kwani VPL ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa
kutafuta matokeo mazuri kuepeuka kushuka daraja.
“Kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto
Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL
2015/2016,” alisema.
No comments:
Post a Comment